July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wadau waanza kutoa maoni maboresho sheria ya uhujumu uchumi Zanzibar

Spread the love

 

WADAU kutoka katika Asasi za Kiraia, wameanza kutoa maoni yao juu ya marekebisho ya Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Maoni hayo yametolewa leo Jumamosi, tarehe 18 Desemba 2021 katika mkutano wa wadau wa Asasi za Kiraia, uliuofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, visiwani Zanzibar.

Mkutano huo umeandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia Tume ya Marekebisho ya Sheria visiwani humo, kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)-Zanzibar na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Zanzibar (ANGOZA).

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Mussa Kombo Bakari, amesema mkutano huo utasaidia kupata maoni yatakayoboresha sheria hiyo.

“Mapambano dhidi ya rushwa hayawezi kufanikiwa kama players (wachezaji) muhimu kama ninyi, kwa maana ya asasi za kiraia hamtashiriki kikamilifu, kwa hiyo wao wenyewe kutumia utalaamu wao isingekuwa rahisi, pengine mafanikio tunayopata yawezekana hatujapata asilimia kubwa pengine baada ya mkutano huu tunaweza kushauriana tukafika mbali zaidi,” amesema Bakari.

error: Content is protected !!