Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Ajira ni janga la kidunia, nini kifanyike?
Tangulizi

Ajira ni janga la kidunia, nini kifanyike?

Spread the love

 

NI dhahiri sasa kuwa ajira ni tatizo la kidunia. Hakuna ubishi sasa hili ni janga. Nchi zote ulimwenguni zinajaribu kukabiliana na janga hili. Nchi zilizoendelea zinapambana kwa namna yake na nchi zinazoendelea zinapamabana kwa namna yake. Ikumbukwe waadhirika wengi hapa ni vijana. Anaandika Mwandishi Maalum…(endelea).

Kwa kuwa Tanzania siyo kisiwa, janga hili ni bayana. Ukitaka kujua ukubwa wa janga hili hapa nchini ni pale zinapotangazwa nafasi za kazi. Mfano ni hivi majuzi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilipoitisha waombaji wa kazi kwa ajili ya usaili.

Inasemekana waliofika jijini Dodoma kwa ajili ya usaili ni zaidi ya watu elfu kumi na moja! Siku za nyuma kidogo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliitisha usaili kama wa Takukuru na uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ukashiba.

Ukubwa wa tatizo unaongezeka kila mwaka. Hii ni kwa sababu kila mwaka shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu vinazalisha mamia kwa maelfu ya vijana wasio na kazi.

Nini kifanyike? Kwa kuwa hii ni nguvu-kazi ya Taifa, ni wakati muafaka sasa Serikali ikachukua hatua za makusudi za kukabiliana na janga hili. Hatua hizi zikichukuliwa kwa umakini ni dhahiri kuwa Taifa litawarudishia vijana matumaini.

Serikali ilete muswada Bungeni au wizara inayohusika na ajira na vijana itengeneze kanuni zitakazozielekeza taasisi za umma na taasisi binafsi kuwapokea vijana walio tayari kujitolea kufanya kazi na taasisi hizo kwa lengo la kupata uzoefu na kupanua uelewa.

Aidha, taasisi hizi zitengeneze utaratibu maalum wa kuwapa kifuta jasho (nauli na chakula cha mchana) vijana hawa. Mafunzo haya yawe ni kwa muda walao wa mwaka mmoja mmoja ili kutoa nafasi kwa vijana wengine. Mafunzo haya yawe ni ya hiari kwa wale tu wanaopenda kufanya hivyo.

Shule, Vyuo, Viwanda, hospitali, vituo vya afya, kampuni za mawasiliano, kampuni za madini, kampuni za utalii, taasisi za umma, Bunge, Mahakama kutaja kwa uchache zinaweza kutoa mafunzo kwa vitendo kwa vijana kati ya 100,000 hadi 200,000 kila mwaka.

Kwa upande wa Serikali, Wizara iunde kitengo maalum cha kuratibu zoezi zima kuanzia Serikali Kuu, Serikali za Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Manispaa na Sekta binafsi. Aidha, utenezwe utaratibu wa kupatiwa ruzuku kulingana na idadi ya vijana waliochukuliwa na taasisi husika kwa upande wa taasisi za serikali, na utaratibu wa kusamahewa baadhi ya kodi kwa taasisi za sekta binafsi kulinga na idadi ya vijana waliochukuliwa.

Kwa kufanya hivi, vijana wengi watajipatia ujuzi, uzoefu, uzamivu na mawanda mapana ya mahusisano na mafahamiano. Aidha, watajenga moyo wa uzalendo kwa taifa lao, na dhana sahihi na imara ya kujiajiri. Kwa wale watakaoajiriwa, ile hoja ya sifa ya mwombaji kuwa awe na uzoefu wa muda fulani itakosa mashiko.

Mwandishi wa Makala hii ni Prosper Minja anapatikana kwa +255 713 123 254 na minjaprosper@gmail.com

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!