October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo Chadema afutiwa kesi, akamatwa tena

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee la chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Hashim Issa Juma, amekamatwa na Jeshi la Polisi, muda mfupi baada ya kuachwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Tukio hilo limetokea leo Jumatano, tarehe 23 Februari 2022, muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, kumuondolea mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yanamkabili.

Heshima Mwasipu, wakili anayemtetea Mzee Juma, amedai hadi sasa sababu za kukamatwa tena kwa mteja wake hazijulikani.

Amedai, bado wako mahakamani hapo ili kujua sababu za Mzee Juma kukamatwa na Jeshi la Polisi, baada ya kuachw ahuru.

“Wamemuachia huru na kumkamata tena, sababu hazijulikani,” amedai Wakili Mwasipu.

Mapema leo, mbele ya Hakimu mkazi, Mbuya, Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono, aliieleza mahakama hiyo kuwa, mkurugenzi wa mashita (DPP) kwa kutumia mamlaka aliyopewa amemuondolea mashtaka hayo.

Katika kesi hiyo, Mzee Issa alikuwa anakabiiwa na mashtaka mawili ya uchochezi, ambayo ni kuchapisha taarifa ya uongo kwa njia ya kompyuta na kusambaza katika mtandao wa Youtube, kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro.

Alikuwa anadaiwa kumtuhumu IGP Sirro kuwa ni gaidi namba moja nchini Tanzania na fisadi, wakati si kweli.

Shtaka la mwisho lililokuwa linamkabili ni uchochezi kinyume na kifungu cha 52 (1) na 53 (1), cha Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari, kufuatia kumuita IGP Sirro ni gaidi namba moja na fisadi, mitandaoni.

error: Content is protected !!