Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TCRA yatangaza kiama waotuma ‘sms’ kujiunga Freemason
Habari Mchanganyiko

TCRA yatangaza kiama waotuma ‘sms’ kujiunga Freemason

Spread the love

 

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema, inafuatilia wale wote ambao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi ‘sms’ wa kuwashawishi watu kujiunga na Freemason. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 22 Februari 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Jabir Bakari katika kikao kati ya mamlaka hiyo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.

Dk. Bakari alikuwa akijibu swali la mmoja wa wahariri, aliyetaka kujua kama laini zote za simu zimesajiliwa, kwa nini hao wanaotuma ‘sms’ hizo hawachukuliwi hatua.

Akijibu kwa kifupi, Dk. Bakari amesema, “tuko kazini kwenye hilo tuacheni.”

Aidha, mkurugenzi huyo amesema, hadi kufikia Desemba 2021, laini zote za simu zimesajiliwa “kwa hiyo hakuna uhalifu unaoweza kufanyika tusimjue. Laini zote zimesajiliwa na kama kuna changamoto mbalimbali, tunazifanyia kazi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!