Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Ajali ya ndege Colombia: Mama aliwaambia watoto wamuache na waende kutafuta usaidizi
HabariKimataifaTangulizi

Ajali ya ndege Colombia: Mama aliwaambia watoto wamuache na waende kutafuta usaidizi

Spread the love

WANAJESHI wa Colombia wanahudumia watoto hao wanne muda mfupi baada ya kupatikana, Wanajeshi wa Colombia wanahudumia watoto hao wanne muda mfupi baada ya kupatikana,MAMA wa watoto wanne waliookolewa baada ya siku 40 kwenye msitu wa Amazon alikuwa hai kwa siku nne baada ya ndege yao kuanguka.

Watoto hao wamepatikana wakiwa hai baada ya kunusurika kutokana na ajali ya ndege na kukaa kwa wiki kadhaa wakijihudumia katika msitu wa Amazoni nchini Colombia.

Magdalena Mucutuy – mama wa watoto hao – aliwaambia watoto wake waondoke wakatafute msaada huku akiwa amelala hana cha kufanya.

Yeye paomoja na marubani wawili wa ndege hiyo, walifariki dunia wakati ndege yao ilipoanguka msituni tarehe 1 Mei mwaka huu.

Kundi lililotoweka likawa kitovu cha oparesheni kubwa ya uokoaji iliyohusisha makumi ya wanajeshi na watu wa eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, baba wa watoto hao, Manuel Ranoque, alisema binti yake mkubwa alimwambia mama yao aliwataka “watoke nje” na kujiokoa.

Ndugu hao wenye umri wa miaka 13, tisa, mitano na mmoja waliokolewa na kusafirishwa kwa ndege kutoka msituni Ijumaa iliyopita.

Walihamishiwa katika hospitali ya kijeshi katika mji mkuu wa taifa hilo Bogota, ambapo gari la wagongwa liliwapeleka hospitali kuu kwa matibabu zaidi.

“Jambo moja ambalo [Lesly mwenye umri wa miaka 13] amenielewesha ni kwamba, kwa hakika, mama yake alikuwa hai kwa siku nne,” Ranoque aliwaambia wanahabari nje ya hospitali.

“Kabla hajafa, mama yao aliwaambia kitu kama, ‘Nyinyi nyinyi ondokeni hapa. Nyinyi mtaona baba yenu ni mtu wa aina gani, na atawaonyesha upendo wa aina ile ile ambao nimewaonyesha,” alisema.

Maelezo yamekuwa yakiibuka kuhusu wakati wa watoto hao msituni na uokoaji wao wa kimiujiza – ikiwa ni pamoja na mambo ya kwanza ambayo watoto walisema walipopatikana.

Mfanyakazi wa uokoaji, Nicolas Ordonez Gomes alikumbuka wakati walipogundua watoto hao.

“Binti mkubwa, Lesly, akiwa na mtoto mdogo mikononi mwake, alikimbia kuelekea kwangu. Lesly alisema: ‘Nina njaa,'” aliambia kituo cha matangazo ya umma RTVC.

“Mmoja wa wavulana wawili alikuwa amelala chini. Aliinuka na kuniambia: ‘Mama yangu amekufa.'”

Alisema waokoaji walimjibu kwa “maneno mazuri, wakisema kwamba sisi ni marafiki, kwamba tulitumwa na familia.”

Ordonez Gomes alisema mvulana huyo alijibu: “Nataka mkate na soseji.”

Katika picha zilizotolewa Jumapili za uokoaji wa watoto hao, ndugu hao wanne walionekana kudhoofika kutokana na wiki walizotumia kujihudumia nyikani.

Bi Mucutuy na watoto wake walikuwa wakisafiri kwa ndege ya Cessna 206 kuelekea Araracuara, katika jimbo la Amazonas, hadi San José del Guaviare, tarehe 1 Mei wakati ilipotoa tahadhari kwa ajili ya hitilafu ya injini.

Kufuatia kuokolewa kwa watoto hao, Rais wa Colombia, Gustavo Petro alisema, ni “furaha kwa nchi nzima. Kuwapata watoto hawa “ni muujiza.”

Aliongeza: “Walikuwa peke yao, wao wenyewe walipata mfano wa kuishi ambao utabaki katika historia.

Rais Petro alishiriki picha ya wanajeshi kadhaa na jamii ya wenyeji wakiwahudumia ndugu, ambao walikuwa wametoweka kwa siku zote hizo 40.

Alisema watoto hao walikuwa wakipokea matibabu – na kwamba alikuwa amezungumza na babu yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!