Saturday , 13 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ajali adui namba 3 wa sekta ya Afya
AfyaHabari MchanganyikoTangulizi

Ajali adui namba 3 wa sekta ya Afya

Moja ya ajali zilizotokea nchini mwaka huu
Spread the love

MKUU wa mkoa wa Morogoro Dk. Steven Kebwe amesema, matukio ya ajali za barabarani yameshika nafasi ya tatu kwa kuwa adui mkubwa wa afya hapa nchini, anaandika Christina Haule.

Dk. Kebwe amesema hayo akifungua warsha ya siku tatu ya masuala ya usalama barabarani kwa waandishi wa Habari wa mkoa wa Morogoro na Dodoma iliyoandaliwa na Chama Cha waandishi wa Habari Wanawake TAMWA kwa ufadhili wa Ushirikiano wa usalama barabarani duniani iliyofanyika mkoani hapa.

Amesema kufuatia ajali kwa sasa kuwa ni adui mkuu wa 3 upande wa sekta ya Afya nchini, adui wa kwanza mkuu ni Magonjwa ya kuambukiza ikifuatiwa na magonjwa yasiyoambukizwa, elimu ya kutosha inapaswa kutolewa kwa jamii hasa madereva kupunguza ajali hizo.

Ungezeko la ajali za barabarani zinapelekea sekta hiyo ya Afya kutumia madawa mengi kwa ajili ya kuwatimu majeruhi wanaotokana na ajali hizo, ambazo zingeweza kutumika katika kutatua matatizo mengine ya kiafya.

Hata hivyo Dk. Kebwe amekubalina na mkakati wa wadau wa kubalidisha sheria ya makosa ya usalama barabarani ya mwaka 1973 inayotumika kwa sasa ili iweze kuleta manufaa kwa kupunguza majanga ya ajali za barabarani nchini.

Aidha amesema, ajali za barabarani zimeendelea kupungua kutokana na mipango mbalimbali inayoendelea kufanywa na kufanya katika kipindi cha mwezi Januari – Machi, 2016 jumla ya ajali 56 zilitokea huku Januari hadi Machi, 2017 ajali 22 zilitokea na kufanya kupungua kwa ajali kwa 11% zilizotokea kwa vyombo vya moto.

Amesema kuwa katika ajali hizo na miezi hiyo kwa mwaka 2016 ajali 42 zilisababisha vifo ambapo mwaka 2017 ajali 17 zilisababisha vifo ambapo vifo vimeonekana kupungua kutoka 54 mwaka 2016 hadi kufikia 20 mwaka 2017 sawa na punguzo la 34%.

Hata hivyo Dk. Kebwe amesema, mpaka sasa jumla ya barabara za lami 15,000 zinazungumziwa kukamilika kwa sasa dhidi ya 11,000 zilizokuwepo lengo likiwa ni kupunguza ajali za barabarani.

Dk. Kebwe amewaasa wanahabari kuyatumia mafunzo hayo vyema ili kuelimisha jamii wakiwemo madereva kuweza kuepuka ajali na kufanya nchi kuendelea kupiga hatua za maendeleo.

Naye Mratibu wa mradi wa usalama barabarani kwa wanahabari, Gladnes Munuo amesema kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) vifo vya ajali za barabarani vimeweza kupoteza watu mil 1.25 katika kipindi cha mwaka 2015.

Munuo amesema kuwa vifo hivyo huwakuta zaidi watu wenye umri wa kati ya miaka 15-29 na kwamba wanaotembea kwa miguu wana asilimia 22 ya kuwa hatarini kupata ajali, wenye baiskeli wana asilimia 4 na wenye pikipiki wana asilimia 23 na kwamba watu 20 hadi 50 wamekuwa wakipata majeraha na ulemavu wa kudumu katika maisha yao.

Pia amesema, Umoja wa Mataifa (UN) umewekwa mkakati wa kupambana na ajali za barabarani duniani na kwamba madereva wametakiwa kuwa makini na kujiepusha na ajali zinazoepukika.

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kuanika mawaziri wanaomtukana Samia

Spread the loveMKUU Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka watu wanaowatuma mawakala...

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

error: Content is protected !!