Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Agizo la Samia kwa kijana shujaa wa ajali ya ndege latekelezwa
Habari Mchanganyiko

Agizo la Samia kwa kijana shujaa wa ajali ya ndege latekelezwa

Spread the love

 

AGIZO la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa jana kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba kijana mvuvi- Majaliwa Jackson apatiwe nafasi mafunzo kwenye Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, limetekelezwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Bukoba … (endelea).

Kijana huyo alijitosa katika Ziwa Victoria na kufanikiwa kuokoa watu 24 waliokuwa kwenye ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka asubuhi tarehe 6 Novemba, 2022 wilayani Bukoba mkoani Kagera.

Licha ya watu 24 kuokolewa wakiwa hai katika ajali hiyo, jumla ya watu 19 walipoteza maisha akiwa rubani wa ndege hiyo na msaidizi wake.

Aidha, taarifa iliyotolewa kwa Umma na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, SACF Puyo Nzalayaimisi imeema Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna John Masunga kijana huyo anatarajiwa kuanza mafunzi ya zimamoto na uokoaji pamoja na ya uaskari katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo wilayani Handeni mkoani Tanga.

“Majaliwa alionesha ujasiri wa hali ya juu kwa kuokoa wahanga 24 wa tukio hilo,” imesema.
Aidha, imesema Kamishna Jenerali anatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za umma, binafsi pamoja na wananchi wa mkoa wa Kagera kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika zoezi la uokoaji katika ajali hiyo.

Pia anatoa pole kwa wafiwa wote na kuwaombea faraja katika kipindi hiki kigumu wanachopitia na anawatakia majeruhi wote afya njema.

“Anawasihi wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kuokoa maisha ya watu na mali dhidi ya majanga mbalimbali,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!