Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili
Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Dk. Eliezer Feleshi
Spread the love

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati ya Maadili ya Mawakili, kuwachukulia hatua mawakili wanaokiuka maadili yao pamoja na kuipotosha mahakama katika utoaji maamuzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Feleshi ametoa agizo hilo leo tarehe 1 Disemba 2023, katika hafla ya kuwapokea na kuwakubali mawakili wapya 279, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Natoa wito kwa kamati ya maadili ya mawakili kuendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kwa mujibu wa utaratibu ulioanishwa katika kifungu cha 13 cha Sheria ya Mawakili na kanuni zote za maadili na mienendo ya mawakili, dhidi ya mawakili wa kujitegemea wanaoharibu heshima ya taaluma ya sheria kwa kukosa uadilifu na maadili dhidi ya mawakili vishoka,” amesema Dk. Feleshi.

Dk. Feleshi amewataka mawakili kufanya kazi zao kwa uadilifu kwa kuwa majukumu yao ni nyeti yanayotegemea kuiongoza mahakama kutenda haki.

“Mkiwa kama mawakili mnapaswa kutambua jukumu la kutoa haki ni sehemu muhimu ya maendeleo ya nchi na watu wake katika kuimarisha utawala wa sheria na misingi ya utawala bora. Ibara ya 107A(1) ya katiba ya Tanzania imebainisha kuwa mamlaka yenye kauli ya mwisho katika utoaji haki Tanzania itakuwa mahakama,” amesema Dk. Feleshi na kuongeza:

“Nawakumbusha kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya mawakili wa kujitegemea kujihusisha na vitendo vya rushwa, udanganyifu kwa maslahi yao binafsi, ikiwemo kuwasaliti wateja wao kwa kupokea rushwa, kutohudhuria mahakamani, kutotunza siri za mteja na kutokuwa na uhusiano mzuri na mteja.”

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Wakili Harlod Sungusia, amewataka mawakili hao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria pamoja na kuhuisha leseni zao za uwakili kwa wakati. Pia, amewataka mawakili wafanye kazi bila woga.

“Miongoni mwa mambo yasiyovumilika ni kufanya kazi bila kuzingatia sheria. Tutahakikisha wanachama wanahuisha leseni zao kwa wakati. Nahimiza kuhakikisha mnafanya kazi zenu mkiwa na leseni halali, msisahau vita dhidi ya ukiukwaji wa maadili ya uwakili imepamba moto, naimani mmefundishwa juu ya muhumu wa kuzingatia maadili,” amesema Sungusia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!