Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ado Shaibu: Tandahimba imesahaulika japo…
Habari za Siasa

Ado Shaibu: Tandahimba imesahaulika japo…

Spread the love


SERIKALI imekumbushwa wajibu wa kikatiba wa kurahisisha na kuharakisha maendeleo ya wananchi kwa kuwajengea miundombinu imara bila ya kuchelewa. Anaripoti 
Jabir Idrissa, Tandahimba … (endelea).

Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado alipokutana na viongozi na wanachama wa chama hicho akiwa kwenye siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Mtwara na Ruvuma, akianzia na Wilaya ya Tandahimba, Mtwara.

Ado amesema serikali inapochelewa kujenga miundombinu ambayo ndio mbolea ya kuchochea morali na kasi ya wananchi kujiletea maendeleo yao, ijue inakwamisha jitihada za kukuza uchumi wa mtu mmoja-mmoja na ule wa taifa kwa ujumla.

Alitolea mfano wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, akisema mpaka sasa haijaunganishwa kwa barabara za lami licha ya mchango wake muhimu katika kukuza Pato la Taifa (GDP) kwa kuzalisha zaidi ya asilimia 40 ya korosho ambayo ni moja ya mazao makuu ya biashara yanayoipatia nchi fedha nyingi za kigeni.

Kiongozi huyo ambaye juzi tu aligombea nafasi kwenye Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alisema  chama hicho kipo katika mageuzi ya kujiendesha kisasa ili kukiwezesha kupata mafanikio makubwa kwenye chaguzi hizo.

Aliwaambia wanachama alipofika Kijiji cha Mdimba, jimboni Tandahimba alikoanzia ziara ya “Kata kwa Kata” kwamba mwisho wa mwaka huu chama kitazindua ofisi yake mpya na ya kisasa ya makao makuu itakayoakisi uendeshaji makini wa shughuli zake nchi nzima.

 

“Baada ya hapo kutakuwa na Operesheni za kishindo za ujenzi wa chama maeneo mbalimbali, Bara na Zanzibar, kutoa mwelekeo wa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025. Tumedhamiria kuziteka siasa za Tanzania.”

“Zaidi ya asilimia 40 ya korosho zote nchini zinazalishwa Tandahimba. Lakini wilaya hii haijaunganishwa kwa barabara za lami na haina maji ya uhakika. Hapa ni muhimu serikali ikaonesha wajibu wake ipasavyo,” alisema.

“Kuhusu maji, nilipopita hapa mwanzoni mwa mwaka huu, nilikuta hali mbaya sana. Nikamtafuta Waziri wa Maji Juma Aweso ambaye baada ya kumweleza alinieleza mpango wa kuukarabati mradi mkubwa wa Makonde. Katika kufuatilia kabla ya kuja safari hii, amesema tayari mkandarasi ameanza kazi. Hii ni hatua nzuri ila sitachoka kuulizia,” alisema.

Ado amesema chama kupitia kwa Waziri wake kivuli wa maji, kitafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo “muhimu sana kwa maendeleo ya  Tandahimba, Newala na mkoa wenyewe wa Mtwara.”

Akizungumzia mipango ya kuhuisha shughuli za kiutendaji ACT Wazalendo, Katibu Mkuu amesema mapinduzi makubwa yanatarajiwa kufanyika katika mpango kabambe wa kukiandaa chama na kushiriki kwa ufanisi uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu taifa wa 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma, Janeth Rithe, Katibu Mkuu mbali na Jimbo la Tandahimba, karima ziara yake hiyo ya “Kata kwa Kata” majimboni, atafika majimbo ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini lengo likiwa ni kuimarisha uhai wa ACT Wazalendo.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!