November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mabalozi wa ‘Rafiki briquettes’ wageuka kivutio maonesho ya madini Geita

Spread the love

 

MABALOZI wa mkaa mbadala wa Rafiki Briquette kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wamekuwa kivutio katika Maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini- 2022 yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Hatua hiyo inakuja baada ya wakazi na wadau mbalimbali wanaoshiriki na kutembelea banda la STAMICO kuwa na kiu ya kutaka kuufahamu vema mkaa huo mbadala ambao unatangazwa na mabalozi hao

Katika maonesho hayo ya mwaka huu ambayo yanafanyika kuanzia tarehe 27 Septemba hadi 8 Oktoba mwaka huu, STAMICO wamekuja na mbinu mpya ya kuonesha ubora wa mkaa huo kwa kutumia kuupikia ili waone ubora wa mkaa huu.

Meneja Masoko na Uhusiano wa STAMICO, Geofrey Meena ameeleza kuwa mkaa huo ambao unauzwa Sh 1,000 kwa kilo moja, una uwezo wa kutumika kupika mara tatu ya mkaa wa kuni.

Amesema mkaa huo uliobuniwa na Shirika kwa kushirikiana na wadau wengine, unatengenezwa kwa makaa ya mawe pamoja na malighafi nyingine.

Ameongeza kuwa mkaa huo utapunguza matumizi ya kuni ambayo yanachangia uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji wa miti kiholela.

Maonesho hayo ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya “Madini na fursa za uchumi ajira kwa maendeleo endelevu.”

error: Content is protected !!