Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yatimiza miaka sita, Zitto atoa ujumbe
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yatimiza miaka sita, Zitto atoa ujumbe

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha siasa cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania leo Jumanne tarehe 5 Mei 2020 kinaadhimisha miaka sita tangu kiliposajiliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

ACT-Wazalendo kilipata usajili wa kudumu tarehe 5 Mei 2014. Kilishiriki uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015.

Katika uchaguzi huo, kilisimamisha wagombea ubunge kwenye maeneo mbalimbali nchini na kufanikiwa kushinda jimbo moja la Kigoma Mjini linaloongozwa na Zitto Kabwe.

Pia, kilishinda nafasi ya udiwani kwenye maeneo kadhaa ikiwamo Kigoma Ujiji hali iliyokifanya kuongoza Halmashauri ya Kigoma Ujiji.

https://twitter.com/actwazalendo/status/1257420284291842051?s=21

Katika salamu zake alizozitoa leo Jumanne kuadhimisha miaka sita, Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama hicho amesema imekuwa miaka sita ya kupigania makundi mbalimbali ya Watanzania bila kuchoka.

Salamu hizo za Zitto zinasema;

Miaka 6 ya majaribu mengi katika maisha yetu ya kila siku, #Watanzania. ACT Wazalendo tumekuwa upande wa Wananchi muda wote, wakati wote bila kujali athari zitakazotupata (Consequences).

▪︎ Tumekuwa na #Wazanzibari walipoporwa haki yao ya kuchagua Kiongozi wanayemtaka!

▪︎ Tumekuwa na #Wakulima wa Mbaazi, Korosho, Pamba, Tumbaku na Karafuu walipoharibiwa masoko ya Bidhaa zao na kudhulimiwa Fedha zao zinazotokana na jasho lao.

▪︎ Tumekuwa na #Wavuvi wa Baharini na Ziwani walipochomewa nyavu zao na kuharibiwa maisha yao.

▪︎ Tumekuwa na #Wafugaji walipovamiwa kuondolewa maeneo ya malisho ya Mifugo yao.

▪︎ Tumekuwa na #Wafanyabiashara walipobambikiwa Kodi kubwa, kutolipwa Fedha zao za marejesho na kufunguliwa kesi za utakatishaji.

▪︎ Tumekuwa na #Wanaharakati wa Haki za Binaadamu na #Waandishi wa Habari wanapobambikiwa kesi na kuwekwa jela, kutekwa, kupotea na hata kuuwawa.

▪︎ Tumesimamia #Uhuru wa Taasisi za Uwajibikaji kama #CAG na kuhakikisha Katiba ya Tanzania inalindwa na kuheshimiwa.

▪︎ Tumekuwa na #Wanasiasa wenzetu wanapoonewa na kunyimwa haki zao bila kujali Vyama vyao.

▪︎ Tumekuwa na #Wananchi kuwaelemisha kujikinga na virusi vya #Corona ili kuzuia vifo vya Watu wetu na kuiwajibisha Serikali kwa kushindwa kuongoza vyema Vita dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19.

Kila mwenye kuonewa, kudhulumiwa na kukandamizwa anasikia sauti ya #ACTWazalendo bila kujali chama chake, Dini yake, kabila lake wala hali yake. Hakika, ULIPO TUPO!

#ACTWazalendo ni Chama cha Watu. Ni Chama chako. Ni Chama chenu. Ni Chama chetu. Leo kinatimiza Miaka 6 tangu kusajiliwa kwake hapo tarehe 5 Mei 2014.

ACT Wazalendo itaendelea kuwa upande wa Wananchi. Ninaomba tuendelee kwa mshikamano kupigania uchaguzi huru wa haki na unaoaminika.

Ninaowaomba muipe dhamana ACT Wazalendo ili ijenge Tanzania inayopaa Kiuchumi, yenye Watu wenye Raha na Furaha #KaziNaBata

Miaka 6 ya Utetezi wa Wananchi: Happy Birthday #ACTWazalendo 5-5-2020

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!