July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo yataka mapendekezo kikosi kazi cha Rais yaheshimiwe

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeshauri maoni na mapendekezo yatakayotolewa na Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia kwa ajili ya kutafuta muarobaini wa changamoto za demokrasia ya vyama vingi nchini, yaheshimiwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 18 Juni 2022 na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji, akizungumza katika kongamano la tume huru kuelekea katiba mpya, lililofanyika Songea, mkoani Ruvuma.

Mwanasiasa huyo mkongwe, amesema wito wa mapendekezo hayo kuheshimika na kutekelezwa kama yatakavyotolewa, ameufikisha kwa wakuu wa nchi, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi.

“Mara hii kiko kazi na yale yatakayofahamika basi yaheshimike ili Wazanzibar na Watanzania wakapige kura kwa salama na amani, iwe atakayechaguliwa aapishwe na apewe madaraka,” amesema Babu Duni.

Mwenyekiti huyo wa ACT-Wazalendo, amewataka Watanzania washikamani katika kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.

“Lazima tushikamane tudai tume huru na katiba mpya ili mabaidiliko yatakapotokea nchi hii ndiyo itakuwa na maendeleo. Kuna kipindi tunataka mabaidiliko ili ACT-Wazalendo tuingie Ikulu hapana, tunataka mabadiliko ya nchi yetu,” amesema Babu Duni.

error: Content is protected !!