Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo walinda kiti Mtambwe
Habari za SiasaTangulizi

ACT Wazalendo walinda kiti Mtambwe

Spread the love

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimelinda kiti cha uwakilishi jimboni Mtambwe lakini kimelalamikia mbinu chafu za makada wa Chama Cha Mapinduzi zilizolenga kulazimisha ushindi upande wao. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika Jumamosi hii kutafuta kiongozi wa kuziba nafasi ya mwakilishi aliyechaguliwa mwaka 2020, mgombea wake, Dk. Mohammed Ali Suleiman, alitangazwa mshindi kwa kupata kura 2449.

Dk. Mohammed alimpita Hamad Khamis Hamad aliyegombea kwa tiketi ya CCM, akitangazwa kupata kura 1531.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, Othman Khamis Othman, alitangaza kuwa wagombea washiriki katika uchaguzi huo walikuwa Said Nassor Hemed wa Chama cha Wamanchi (CUF) aliyepata kura 43 na Mohamed Masoud wa Chama cha CHAUMA aliyepata kura 22.

Taarifa ya Msimamizi wa Uchaguzi huyo inaonesha kuwa watu walioandikishwa kuwa wapigakura jimbo la Mtambwe ni 6098.

Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma wa ACT Wazalendo, Salim Abdalla Bimani amesema uchaguzi huo ulijaa visa na mbinu nyingi chafu zilizolenga kulazimisha CCM kushinda.

Akizungumzia matokeo yaliyotangazwa na hususan kura A mgombea wa CCM, Bimani alisema ni kura za hila na mgombea huyo angezidishiwa kura zaidi ya hizo na akatangazwa mshindi lakini “tulipambana vya kutosha kuzuia hila.”

Naye Mratibu wa ACT Wazalendo kisiwani Pemba, Said Ali Mbarouk alisema kwa uchaguzi ulivyoendeshwa, ni dhahiri CCM wameendelea na utaratibu wao wa kutafuta ushindi kwa hila.

“Tunayo shida kubwa kwenye uendeshaji wa uchaguzi. Kwa mfano Sekretariat ya ZEC ilipanga wasimamizi wa uchaguzi, wilaya, jimbo, wasimamizi wa vituo vya kura na wasaidizi wao wakiwa wakereketwa wa CCM walio wakorofi, na ambao wamewezesha kuibwa kura.

“Kuruhusu mapandikizi kupiga kura wasio wenyeji wa jimbo. Kugawa kura hewa zaidi ya moja kwa makada wao, wengine wakipewa kura hadi tano na kuzipiga kwa mgombea wa CCM na kuwatoa mawakala wa ACT ni miongoni mwa mbinu zao,” alisema.

Taarifa zaidi kutoka vyumba vya kuhesabia kura zinasema kutolewa nje kwa mawakala wa ACT kulifuatiwa na kuingizwa kura hewa zilizopigwa kabla na kura nyengine hewa zilizopigwa akitiliwa mgombea wa CCM, pamoja na kukwepa utaratibu wa hesabu ya kura kuanza kwa kuhakiki vishina vya kura zilizopigwa, hatua iliyo ya ukiukaji sheria ya uchaguzi.

Wananchi wa Mtambwe walipiga kura kuchagua Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kufuatia kifo cha mwakilishi waliyemchagua kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Habibu Mohamed.

Rekodi za uchaguzi kwenye Tume ya Uchaguzi Zanzibar, zinaonesha kuwa CCM tangu uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, haijawahi kufikisha kura 400 katika jimbo la Mtambwe.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!