Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo: Wachochezi migogoro ta ardhi wawajibishwe
Habari za Siasa

ACT Wazalendo: Wachochezi migogoro ta ardhi wawajibishwe

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, awawajibishe viongozi wanaochochea migogoro ya wakulima na wafugaji Kwa kushindwa kusimamia vyema matumizi ya ardhi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Alhamisi na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Mkoa was Lindi, Isihaka Mchinjita, ikiwa ni siku Moja tangu mkulima Said Matimbanya, kudaiwa kuuliwa na baadhi ya wafugaji katika Kijiji Cha Kikole mkoani humo.

“Aidha, tunatoa wito kwa Rais Samia kuwawajibisha wateule wake akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, kwa kushindwa kusimamia Mpango wa Matumizi ya Ardhi unaogawanya maeneo ya kilimo na ufugaji na badala yake kwenda kuchochea kutofuatwa mpango huo hali inayopelekea mauaji ya wakulima na wafugaji,” imesema taarifa ya Mchinjita.

Aidha, Mchinjita ametoa wito Kwa watunga sera kuanzisha seraadhubuti zitakazomaliza tati,o la wakulima na wafugaji wa Lindi.

“Tunatoa wito kwa Watunga Sera kuja na sera madhubuti zitakazoondosha tatizo la wakulima na wafugaji mkoani Lindi kwani kutofanya hivyo ni kufuga bomu la mauaji ya kimbali ya wakulima na wafugaji ambayo yananukia mkoani Lindi,” imesema taarifa ya Mchinjita.

Kwa mujibu was taarifa ya Mchinjita, marehemu Matimbanya ameuawa Kwa kushambuliwa na mikuki akiwa shambani kwake, ambapo watuhumiwa hao was mauaji wanadaiwa walipeleka ng’ombe zao zaidi ya 100 shambani humor kwa ajili ya malisho.

“Marehemu Saidi Matimbanya alivamiwa na wafugaji shambani kwake siku ya tarehe 7 Septemba 2022, majira ya saa nne asubuhi. Siku hiyo ya tukio marehemu alikwenda shambani kwake akiambatana na ndugu yake na kuwakuta ng’ombe zaidi ya 100 wakichungwa na kula ndani ya shamba lake na akina mama wa kimang’ati. Saidi alipokuwap akiwahoji wafugaji hao wa kike, ghafla walijitokeza wafugaji wa kiume na kumshambulia kwa mikuki na kumuua,” imesema taarifa ya Mchinjita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!