Thursday , 9 May 2024
Home Kitengo Michezo Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili
Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the love

WAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa Bwana Wastahili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Video ya wimbo huo imeachiwa leo tarehe 18 Machi 2024 saa mbili usiku na  imerekodiwa katika Studio ya Flying Wave Studio na kuongozwa na Director maarufu ajulikanae kama Director Joowzey.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya video hiyo kuachiwa hewani (kuzinduliwa) Mwenyekiti wa Gethsemane Group Kinondoni GGK, Geoffrey Joseph amesema ni furaha kwao kuja na video ya wimbo huo ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumtukuza Mungu.

“Ujumbe mkubwa kwenye wimbo huu ni kwamba Mungu pekee ndie anastahili kuabudiwa na yeye ndiye anatosha kwa kila kitu hasa kipindi hiki ambacho baadhi ya madhehebu wapo Kwenye mfungo, tunaamini wimbo huu ni ibada na utawasogeza karibu zaidi na Mungu,” amesema Joseph.

Aidha, ametoa neno kwa wasikilizaji na watazamaji wa video ya wimbo huo kutambua hakuna yoyote anayestahili kuabudiwa zaidi ya Mungu pekee. https://youtu.be/P5PRVczx388?si=hmcj9VNA68vvRztQ

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

error: Content is protected !!