Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu amesema aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, alikuwa mpole na mkarimu enzi za uhai wake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Lissu ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumzia kifo cha Mzee Mwinyi kilichotokea Alhamisi tarehe 29 Februari 2024.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, jana Jumapili, Lissu amesema Mzee Mwinyi pamoja na mke wake, Mama Sitti Mwinyi, walimtembelea hospitalini Nairobi nchini Kenya, alikokuwa anapatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana.
“Rais Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia siku ya Alhamisi na kuzikwa jana (Jumamosi) alikuwa mpole na mkaribu. Nilipopigwa risasi Septemba 17 na kukimbizwa Nairobi kwa matibabu, Mzee Mwinyi na mama Sitti walikuwa Hospitali ya Nairobi kunitakia nafuu ya haraka. Apumzike kwa amani ya milele,” ameandika Lissu.
Lissu alilazwa hospitali jijini Nairobi Septemba 2017, baada ya kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana, nyumbani kwake Dodoma.
Leave a comment