Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Hofu chanzo viongozi vyama upinzani kugoma kung’atuka
Habari za SiasaTangulizi

Zitto: Hofu chanzo viongozi vyama upinzani kugoma kung’atuka

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo anayemaliza muda wake, Zitto Kabwe amesema hofu ndizo zinazowafanya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani kugoma kutoka madarakani, kitendo alichotaja kuwa kinadhoofisha utendaji wa vyama vyao kwa kuwa havijengwi kitaasisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Zitto ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Machi 2024, akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds, baada ya kuulizwa maoni yake juu ya viongozi hao wanaogoma kung’atuka kwa maelezo kuwa wanaogopa vyama vyao kuhujumiwa.

“Nadhani ni hofu ambazo zinaweza kuwa na hoja, lakini hazina msingi kwa sababu tunachotakiwa ni kuimarisha taasisi za chama. Kila chama cha siasa kina njia zake za kutambua watu mabao wanapenya hamna taasisi ambayo haipenyezi hata sisi CCM tunapenyeza watu kama wao wanavyofanya.

“Muhimu ni chama kimejenga mfumo wa kuwatambua na kuweza kuwaondoa, huwezi kusema eti utakuwa na kiongozi ambaye atakaa muda wote kwa sababu unaogopa CCM watapenya hiyo haiwezekani na hii itafanya udumavu. Kwetu tulichoamua ni kujenga taasisi,” amesema Zitto.

Katika hatua nyingine, Zitto amesema Tanzania kuna changamoto ya watu wanaohubiri demokrasia wakiwa nje ya vyama vyao, lakini ndani hawaiishi hiyo demokrasia.

“Tuna changamoto kubwa hapa Tanzania ya kuwa na watu ambao wanahubiri demokrasia lakini wao wenyewe sio wana-demokrasia akiwa nje demokrasia ni ya nje lakini ndani hata nyumbani kwake hata watoto wake hawana uhuru.

“Familia yake haina uhuru, sasa sisi tunajaribu kwa kadri ya uwezo wetu. Hatusemi kwamba tumefanikiwa kwa asilimia zote tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kujenga utamaduni ndani ya chama chetu ambao una unayatenda ambayo tunayahubiri nje,” amesema Zitto.

Miongoni mwa vyama vya siasa vya upinzani ambavyo baadhi ya viongozi wake wamekaa muda mrefu madarakani ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!