Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha
Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kufuatia vifo vya watu 25 na majeruhi 21 vilivyotokea katika ajali ya gari. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

 Ajali hiyo imetokea jana Jumamosi saa 11 jioni katika barabara kuu ya Arusha – Namanga Ngaramtoni Kibaoni kata ya Orolieni wilayani Arumeru mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mkoa wa Arusha SACP Justine Mascjo, waliopoteza maisha ni wanawake 10, wanaume 14 pamoja na mtoto 1 wa kike wakiwemo raia wa kigeni kutoka mataifa 7 ya Kenya, Togo, Madagascar, Burkina Faso, Afrika ya Kusini, Nigeria na Marekani.

Idadi ya majeruhi ni 21 wakiwemo raia wa kigeni kutoka mataifa ya Nigeria, Ivory Coast, Uswizi, Cameroon, Uingereza, Mali na Hawai.

SACP Mascjo amesema ajali hiyo imehusisha gari la kubeba mizigo la kampuni ya KAYCONSTRUCTION ya Nairobi, Kenya likitokea Namanga kwenda Arusha ambalo liligonga magari matatu.

Chanzo cha ajali ni gari hiyo kupoteza uelekeo na kuyagonga kwa nyuma magari matatu yaliyokuwa yakielekea Arusha ambayo ni daladala aina ya Nissan Caravan yenye kufanya safari zake Arusha mjini kwenda Ngaramtoni na Mercedes Benz Saloon (gari binafsi).

Gari nyingine ni Toyota Coaster mali ya shule ya New Vision iliyopo Ngaramtoni Arusha iliyowabeba raia wa kigeni wanaofanya shughuli za kujitolea kwenye shule hiyo.

“Rais Samia anawapa pole majeruhi wa ajali hiyo pamoja na wafiwa wote na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema Peponi. Amin,” imesema taarifa iliyotolewa leo Jumapili na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Potofu huzaa potoshi/ potoshi huzaa potofu?

Spread the loveDayosisi 7 za KKKT katika kanda ya Ziwa na Magharibi,...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

error: Content is protected !!