Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema aitwanga barua Bunge akidai marekebisho ya katiba
Habari za Siasa

Mbunge Chadema aitwanga barua Bunge akidai marekebisho ya katiba

Aida Khenan
Spread the love

MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Aida Khenani, ameliandikia barua Bunge, kwa lengo la kuonesha kusudio lake la kuwasilisha muswada binafsi wa kudai marekebisho ya katiba, ili kuweka vifungu vitakavyotatua changamoto za kiuchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 8 Februari 2024, nje ya Bunge jijini Dodoma na Khenani, akisema naamini mhimili huo utafanyia kazi maombi yake.

“Nimemwandikia barua katibu wa Bunge kwa kuonyesha kusudi la kuleta muswada binafsi na haki hiyo napata kwenye kanuni zetu za Bunge. jina la muswada litakuwa Muswada wa mabadiliko ya 15 ya katiba wa 2024 ambao wenye lengo la kuhakikisha malalamiko na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi zitafanyia marekebisho,” amesema Khenani.

Khenani amesema amechukua hatua hiyo baada ya kuona robo tatu ya mapendekezo yaliyotolewa na wadau ambao yalikuwa yanagusa marekebisho ya katiba, yameachwa katika miswada ya sheria za uchaguzi iliyopitishwa bungeni, hivi karibuni.

“Zipo sababu ambazo zimepelekea mimi nionyeshe kusudio la kupelekwa muswada huo na kwa sababu ni mara chache sana sote tunajua toka tunapitisha marekebisho ya sheria hizo tatu ambayo ukitazama miswada na maoni yaliyotolewa ukiangalia robo tatu hayajachukuliwa sababu mengi yalilenga maboresho kwenye katiba,” amesema Khenani na kuongeza:

“Naamini Bunge litapokea, Spika Tulia Ackson atapokea, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa alionesha nia kwenye miswada naamini litapokelewa na kufanyiwa kazi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

error: Content is protected !!