Tuesday , 14 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia apangua, ateua wakurugenzi taasisi za umma
Habari za Siasa

Samia apangua, ateua wakurugenzi taasisi za umma

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wanne katika taasisi mbalimbali ikiwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imesema Rais Samia amemtea Dk. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Dk. Bill Kiwia

Kabla ya uteuzi huu Dk. Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira (Biodiversity Conservation) Ofisi ya Makamu wa Rais. Anachukua nafasi ya Dk. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake. Ameongeza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 3 Februari 2024.

Pia amemteua Abdul-Razag Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Kabla ya uteuzi huu Badru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB).

Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba atapangiwa kazi nyingine.

Pia Rais Samia amemteua Dk. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Dk. Kiwia anachukua nafasi ya Badru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Uteuzi huu unaanza leo tarehe 6 Februari 2024.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Mbunge ataka huduma Ultrasound itolewe bure kwa wajawazito

Spread the loveMBUNGE wa Viti Maalum, Esther Malleko, ameitaka Serikali kutoa bure...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CUF yajipanga kuelekea chaguzi zijazo

Spread the loveCHAMA cha Wananchi (CUF), kimejipanga kujijenga kisiasa kuelekea chaguzi zijazo...

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

AfyaHabari za Siasa

Wizara afya kutumia Sh. 1.31 trilioni, huduma za kibingwa zapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Afya, imeliomba Bunge lipitishe makadirio yake ya mapato...

error: Content is protected !!