Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wachunguza kifo mkuu wa kituo aliyedaiwa kuuawa na polisi
Habari Mchanganyiko

Polisi wachunguza kifo mkuu wa kituo aliyedaiwa kuuawa na polisi

Spread the love

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limetangaza kuendelea kufanya uchunguzl wa tuklo la mauaji ya Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Chiungutwa Wilaya ya Masasi, Eliuterius Eliuterius Hyera aliyefariki dunia tarehe 1 Februari mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hyera alifariki wakati akiwa anaendelea kupatowa matibabu katika Hospitali ya Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara baada ya kujeruhiwa kwa risasi.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe Jumapili na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo imeeleza kuwa katika siku hiyo ya tarehe 1 Februari, Hyera alijeruhiwa kwa risasi akiwa ameongozana na askari mwenzake katika ukamatajl wa mtuhumiwa wa tukio la kuvunja oflsi na kulba.

“Mtuhumlwa huyo alianza kukimbia ill asikamatwe ndipo askari aliyekuwa na bastola alipofyatua risasi kwa lengo la kufanikisha ukamataji na ikapelekea kumjeruhi Mkaguzi huyo.

“Juhudi za kuokoa maisha yake illfanyika kwa kupelekwa Hospitall ya Ndanda ambapo alifariki dunia akiendelea na matibabu,” ameeleza Kamanda huyo.

Amesema mwill wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Ndanda kwa uchunguzi zaldi na mtuhumiwa anashikiliwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha, amesema juhudi za kuwasaka watu waliohuslka katika tukio hilo na kuvunja na kuiba, zinaendelea kufanylka ili kuwafikisha mbele ya sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!