Monday , 4 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais wa Namibia amefariki dunia
KimataifaTangulizi

Rais wa Namibia amefariki dunia

Spread the love

HAGE Gengob, Rais wa Namibia, amefariki dunia wakati akipokea matibabu hospitalini katika mji mkuu, Windhoek. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Makamu wa rais Nangolo Mbumba ametangaza kuwa Geingob alifariki Jumapili alfajiri.

Mkewe Monica Geingos na wanawe walikuwa karibu naye,” Mbumba alisema katika taarifa yake.

 Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 aligunduliwa kuugua saratani na alitangaza hali yake mbele ya umma mwezi uliopita.

Ofisi yake ilitangaza kwamba atasafiri kuelekea Marekani kupata matibabu, lakini kwamba atarudi Namibia, tarehe Februari mwaka huu.

Geingob aliapishwa kuwa rais mnamo 2015 na alikuwa anatumikia awamu yake ya pili na ya mwisho uongozini.

Alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka jana, na mnamo 2014 alifichua kuwa amepona saratani ya tezi dume.

Namibia inatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu mwezi Novemba.

Chama tawala cha Swapo ambacho kimekuwa madarakani tangu 1990, kimemteua Bi Nandi-Ndaitwah kama mgombea urais.

Yeye ndiye Waziri mkuu wa sasa na iwapo atashinda, atakuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

Habari za SiasaTangulizi

Kikwete: Mwinyi alinianzishia safari yangu ya kisiasa

Spread the loveRAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema atamkumbuka...

error: Content is protected !!