Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia amlilia Rais Namibia
Habari za SiasaTangulizi

Samia amlilia Rais Namibia

Spread the love

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na kifo cha Rais wa Jamhuri ya Namibia, Dk. Hage Gottfried Geingob kilichotokea leo Jumapili jijini Windhoek nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumapill na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema Rais Samia amekuwa na urafiki wa muda mrefu na Dk. Geingob ambaye alikuwa anamuita kaka.


Rais Samia ametuma salamu za rambirambi kwa niaba ya Watanzania kwa wananchi wa
Namibia, serikali ya nchi hiyo pamoja na mke wa marehemu, Monica Geingob, na familia kwa ujumla.

“Nimesikitishwa sana na msiba wa kaka yangu Rais wa Namibia, Dk. Geingob, ambaye nimemfahamu kuwa kiongozi msikivu, mtu wa watu na amekuwa miongoni mwa alama za ukombozi wa Namibia,” Rais Samia amesema.

Kufuatia undugu na urafiki wa muda mrefu na Namibia, Rais Samia pia ametoa pole kwa uongozi na wanachama wote wa chama tawala rafiki cha SWAPO.

Mara ya mwisho Rais Samia alipokelewa kwa ukarimu mkubwa na Rais Geingob nchini Namibia tarehe 7 Mei 2023 alipokwenda kuhudhuria mkutano wa dharura wa utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika).

Viongozi hao wawili walizungumzia mambo mbalimbali, ikiwemo kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, hususan kisiasa na kiuchumi.

Tanzania na Namibia zimekuwa na uhusiano wa kindugu na wa muda mrefu tangu wakati wa harakati za ukombozi wa Taifa hilo.

“Aidha, uhusiano umeendelea kuimarika zaidi siku hadi siku. Mungu ailaze roho ya Rais Dkt. Hage Gottfried Geingob mahali pema peponi, Amin,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!