Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aadhimisha ‘birthday’ kwa tukio hili
Habari za Siasa

Rais Samia aadhimisha ‘birthday’ kwa tukio hili

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameadhimisha kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa (Birthday) kwa kushiriki kupanda miti inayotarajiwa 4720, katika eneo la ekari 35.7 lililopo Donge Muwanda, Jimbo la Tumbatu , visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imesema Rais Samia amepanda miti hiyo kwa kushirikiana na makundi mbalimbali, leo tarehe 27 Januari 2024, ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

“Aidha, Rais Samia amesema siku hii inaadhimishwa kwa kupanda miti kwa sababu ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira nchini hasa Zanzibar. Amesema upandaji wa miti kwa wingi pamoja na mikoko utasaidia kurudisha hali asilia ya bahari na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa ardhi,” imesema taarifa ya Yunus.

KIatika hatua nyingine, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, kuzuia uchimbaji mchanga holela pamoja na kusitisha shughuli za kukata matofali ya miamba na kutoa vibali vya uchimbaji kwa wananchi wanaokaa maeneo ya juu.

1 Comment

  • Duh!
    Hongera kwa kuhimiza mazingira bora. Pia zitungwe sheria za kuwasweka jela na faini kubwa kwani wanaofanya hivyo ni matajiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!