Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba asema upatikanaji katiba mpya mfupa mgumu
Habari za Siasa

Prof. Lipumba asema upatikanaji katiba mpya mfupa mgumu

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema mapambano ya kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi bado ni mfupa mgumu kwa Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, tarehe 27 Januari 2024, jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba, ugumu huo unatokana na baadhi ya mapendekezo ya wapinzani ambayo Serikali inayoongozwa na CCM imeyakataa hususan yale yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba.

“Pamoja na watu kupoteza maisha kudai Katiba Mpya na Tume Huru za Uchaguzi, Katiba yenye misingi ya demokrasia, tuweze kuwa na utawala bora unaoheshimu haki za binadamu, unaopambana na ufisadi na rushwa, bado mambo haya hatujaweza kufanikiwa,”  amesema Prof. Lipumba.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya hayati John Magufuli, iliweka kando mchakato wa upatikanaji katiba mpya ulioasisiwa na mtangulizi wake, Jakaya Kikwete, hivyo Rais Samia alivyoingia madarakani alionesha matumaini ya kuukamilisha lakini hadi sasa hakuna dalili ya ukamilishaji.

“Sasa alipofariki Dkt. Magufuli na Mama Samia kuwa Rais kufuatana na Katiba sisi tulikuwa na matumaini kwamba ana fursa za kuweza kukamilisha zile ahadi ambazo mwenzake Hayati Rais Magufuli alizitaja ndani ya Bunge kwamba anaweza akazikamilisha,”  amesema Prof. Lipumba

Kauli hiyo ya Prof. Lipumba imekuja baada ya Rais Samia hivi karibuni kuweka msimamo wa serikali yake kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, ambapo alisema utekelezaji wake utatanguliwa na utoaji elimu ya katiba kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!