Saturday , 11 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Kipindupindu chasababisha shule kutofunguliwa Zambia
AfyaKimataifa

Kipindupindu chasababisha shule kutofunguliwa Zambia

Spread the love

Serikali ya Zambia imetangaza kuahirisha kuanza kwa muhula mpya ya masomo kwa wiki tatu zaidi kutokana mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeshaua watu 150 tangu Oktoba, 2023. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Waziri wa Elimu nchini humo, Douglas Syakalima amesema shule nchini humo zilipaswa kufunguliwa tarehe 8 Januari 2024 lakini sasa zitafunguliwa tarehe 29 Januari  2024.

Zaidi ya watu 4,000 wameugua kipindupindu na vifo 150 vimeripotiwa, takwimu za hivi karibuni za Serikali zinaonyesha kiwango cha vifo ni asilimia 3.7.

“Serikali ina wasiwasi kuhusu athari za mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika sekta ya elimu, hivyo hatua hiyo imechukuliwa ili kulinda afya za wanafunzi,” amesema Syakalima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!