Saturday , 11 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB yawazawadia washindi 100 waliobahatika droo ya 7 ya MastaBata
Biashara

NMB yawazawadia washindi 100 waliobahatika droo ya 7 ya MastaBata

Spread the love

BENKI ya NMB imetangaza washindi 100 waliobahatika katika droo ya 7 ya kampeni yake ya MastaBata Halipoi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni hatua ya benki hiyo kuhamasisha na kuongeza furaha na ari ya msimu wa sikukuu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Afisa wa mifumo ya kidigitali wa Benki ya NMB, Rukia Mhendile akichezesha droo ya kumpata mmoja wa washindi wa droo ya saba ya mastabata iliyochezeshwa katika tawi la NMB Mbagala, Dar es Salaam. Kulia ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Irene Kawila na katikati ni Meneja wa Tawi la NMB Mbagala, Halima Charazo.


Akizungumza wakati wa droo ya 7 iliyofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam, Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mbagala, Halima Mcharazo alisema washindi 100 wa benki hiyo waliobahatika watajipatia zawadi ya fedha taslimu 100,000/- kila mmoja na kuongeza kuwa kampeni ya miezi mitatu ya benki hiyo inalenga kuwashukuru wateja wa benki hiyo kwa kuendelea kuwa na imani na benki hiyo.

 Mcharazo alibainisha kuwa zaidi ya wateja 620 hadi sasa wamebahatika kujishindia zawadi za fedha taslimu wakati wa droo za kila wiki na mwezi wakati wa kampeni ya benki hiyo ya MastaBata iliyozinduliwa mnamo Oktoba 27, 2027.

 “Msimu wa kutoa umewadia, na unatupa fursa nyingine ya kuonyesha upendo na shukrani zetu kwa wateja wetu. Kupitia droo ya kampeni yetu ya MastaBata leo, wateja wetu 100 watakaobahatika watajishindia shilingi 100,000 kila mmoja,” Mcharazo alisema.

 Alisema kampeni hiyo inayotarajia kufika kilele Januari 25, 2024, itawawezesha wateja wa benki hiyo kujishindia zawadi za zaidi ya shilingi milioni 350 za fedha taslimu na, safari za mapumziko mwisho wa mwezi  katika fukwe za Kendwa Rocks visiwani Zanzibar pamoja na safari za Cape Town, nchini Afrika Kusini katika droo ya mwisho wa kampeni.

 “Kampeni yetu inalenga kuhaasisha ya malipo ya kidijitali ambayo yameonekana kuwa rahisi zaidi, ya haraka na salama. Kwa mantiki hiyo, nawahimiza wateja wetu wa Benki ya NMB kuendelea kutimia kadi zao za MasterCard wanapolipia bidhaa au huduma kupitia Mashine za Malipo (POS), QR Code au manunuzi ya mtandao ili kupata nafasi ya kushinda pesa taslimu na safari zilizogharamiwa kila kitu na venki wakati wa kampeni,” alisema.

 Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) Irene Kawili wakati wa hafla hiyo alibainisha kuwa droo ya Kampeni ya MastaBata inafanyika kwa kuzingatia kanuni na taratibu za bodi ya michezo ya kubahatisha.

 “Kampeni ya MastaBata inaendeshwa kwa uwazi sana. Ninawahimiza wateja wa benki kuendelea kutumia njia za kidijitali za malipo ya benki ili kuongeza nafasi zao za kushinda,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Biashara

Meridianbet kasino yaja na promo ya mil 200/=

Spread the love  Kimbunga Hidaya kilikuja na madhara makubwa sana katika maeneo...

Biashara

Moon of Thoth, historia ya Misri ya kale ilipofichwa ndani ya kasino

Spread the love  Nchi ya Misri imebeba karibia asilimia kubwa ya mambo...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the loveWADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku...

error: Content is protected !!