Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang
Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the love

SERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya udongo ya Mlima Hanang mkoani Manyara, yaliyosababisha mauji ya watu zaidi ya 50 na kujeruhi wengine 85. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 4 Desemba 2023 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwenda kwa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alipowasili mjini Katesh, wilayani Hanang, kwa ajili ya kushughulikia janga hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana Jumapili.

Amesema uchunguzi huo utakapokamilika utaonesha sababu za mlima huo kuporomosha udongo.

“Wizara ya Madini tumelazimika kuileta kwa haraka tunataka tuone ni nini hiki, aina gani ya udongo huu? mwamba kama ambavyo ilifanyika Mtwara 1990 na tukagundua kulikuwa na mwamba ulilegea hapa baada ya uchunguzi wao tutapata taarifa ni nini hasa kilisababisha hiki,” amesema Waziri Majaliwa.

Hadi sasa Serikali imetuma vikosi vya uokoaji ikiwemo wanajeshi 300 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji.

Waziri Majaliwa ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi katika eneo lililoathirika ili kulinda raia na mali zao, huku akitaka watalaamu wabaki hadi pale hali itakapotengemaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!