Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mlima wa Moto wazindua kongamano la SHILO kumuenzi Rwakatare
Habari Mchanganyiko

Mlima wa Moto wazindua kongamano la SHILO kumuenzi Rwakatare

Spread the love

KANISA la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dar es Salaam, limezindua kongamano liitwalo SHILO kama sehemu ya kumuenzi mwanzilishi wa Kanisa hilo, Hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Uzinduzi wa kongamano hilo la siku nane ambalo hufanyika kila mwisho wa mwaka ulifanyika siku ya Jumapili mara baada ya Ibada kanisani hapo na Askofu wa Kanisa hilo, Rose Mgetta.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kongamano hilo, Askofu Mgetta alisema kongamano hilo liliasisiwa na hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare na limekuwa likifanyika kila mwaka hata baada ya kifo chake.

Askofu Rose Mgeta wa Kanisa la Mlima wa Moto akizungumza kuhusu tamasha hilo la SHILO

“Maombi ya SHILO yalikuwa ni maono ya Askofu wetu mwanzilishi hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare na tumekuwa tukiyaendeleza mwaka hadi mwaka na makanisa yote ya Mlima wa Moto wamekuwa wakifanya maombi haya kila mwaka,” alisema

“SHILO ni majibu ya mwisho ya mtu ambaye amekata tamaa mfano ameshindwa kupata mtoto, ameshindwa kuolewa akija kwenye tamasha hili la siku nane la SHILO lazima jibu lake lipatikane,” alisema

Alisema wataendelea kuombea taifa liendelee kuwa na amani na kuondokana na majanga kama ukame na matatizo mbalimnbali yanayotokea kwenye jamii.

Kwaya ikitumbuiza

“Ili Kanisa liwe na amani lazima nchi iwe na amani kwa hiyo umekuwa wajibu wetu kuhakikisha tunaombea amani ya nchi mara kwa mara na tunamuombea Rais wetu Mungu aendelee kumpa afya njema aweze kuendelea kulikongoza vyema taifa letu,” alisema Askofu Rose

Naye Dk. Rose Rwakatare alisema kongamano la SHILO lilianza miaka 20 iliyopita katika Kanisa hilo lililoko Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

“Hili kongamano tunakuwa nalo kila mwaka na lilianzishwa na marehemu Askofu Dk. Getrude Rwakatare sisi tunaliendeleza kumuenzi na tunaahidi kuendelea kumuenzi situ kwa kongamano hili bali kwa kazi zote alizokuwa akizifanya,” alisema

Washiriki wakiburudika

Alisema Askofu Dk. Getrude Rwakatare aliweka misingi mizuri ya Kanisa na ndiyo sababu limekuwa likiendelea kutoa huduma ya kiroho hata baada ya kuondoka kwake.

“Namshukuru Rose Mgeta kwa kusimamia maono haya na kuhakikisha kazi ya Mungu inaendelea na nashukuru kwa mzigo mkubwaa alionao Rose kuombea taifa hili ni watu wachache wanaojitoa kuombea taifa lakini Rose na kanisa wamesimama kuombea nchi dhidi ya majanga kama ukame,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Spread the loveSERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!