Saturday , 11 May 2024
Home Kitengo Michezo Nyashinski atua Bongo, aahidi makubwa Serengeti Oktoba Fest
Michezo

Nyashinski atua Bongo, aahidi makubwa Serengeti Oktoba Fest

Spread the love

 

NYAMARI Ongegu anayejulikana zaidi kama Nyashinski ameahidi makubwa katika onyesho lake la kesho katika Tamasha kubwa la Serengeti Oktoba Festival litakalofanyika kesho tarehe 21 Oktoba, 2023 katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Lite litakuwa na burudani za kutosha ikiwa vinywaji lakini pia itatoa fulsa kujua tamaduni kutoka katika nchi hizo za Afrika Mashariki na Kati.

Nyashinski ambaye ni msanii wa Hip Hop kutokana nchini Kenya ametoa ahadi hiyo muda mchache mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere tayari kwa ajili tamasha hilo.

“Kesho ni siku kubwa sana kwangu, tangu nikiwa Kenya nilikuwa nafikiria na sikuamini kupata nafasi ya kupanda jukwaa moja na wasanii wakubwa kutoka Afrika Mashariki kama Ali Kiba na Jose Chameleone, mimi ni mshabiki mkubwa wa Chameleone hivyo kuwa naye katika jukwaa moja ni kitu kikubwa sana, alisema Nyashinski na kuongeza:

“Ali Kiba tulianza kitambo sana na nimekuwa nafuatilia nyimbo zake jambo lililonifanya niwe mshabiki wake mkubwa, hivyo itakuwa siku poa sana kushiriki naye kwenye jukwaa moja.”

Nyashinski alisema amejiandaa vya kutosha ikiwa kufanya mazoezi ya kwa ajili ya tamasha hilo, hivyo mashabiki wangu waje Coco Beach kwani watapata kitu bora zaidi.

Tamasha hilo mbali na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki, pia kutakuwa na tamaduni za nchi hizo pamoja na vyakula vya asili kutoka katika nchi hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

Michezo

Unakosaje pesa ukiwa na Meridianbet leo

Spread the love Alhamisi ndio hii sasa mteja wa meridianbet ambapo leo...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

error: Content is protected !!