Friday , 10 May 2024
Home Kitengo Michezo Klabu ya madini yaibuka na medali 4 SHIMIWI, mikakati yaanikwa
Michezo

Klabu ya madini yaibuka na medali 4 SHIMIWI, mikakati yaanikwa

Spread the love

Katika kuhakikisha Klabu ya Michezo ya Madini ( Madini Sports Club) inashiriki michezo kwa mafanikio makubwa   imebainisha mikakati ya kiufundi itakayo leta matokeo bora  katika michezo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mikakati hiyo  imebainishwa leo tarehe 17 Oktoba 2023 na Naibu Katibu Mkuu Madini, Msafiri Mbibo alipomwakilisha Katibu Mkuu Madini katika kikao cha  kupokea taarifa ya ushiriki  wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo  la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI – 2023) jijini Dodoma.

Mbibo amesema kuwa Wizara imefurahishwa na ushindi mlioupata katika mashindano ya SHIMIWI lakini pamoja na ushindi huo Wizara ina mikakati mbalimbali ya kiufundi ikiwemo mpango wa  kushiriki  michezo  mbalimbali katika ngazi ya mkoa na taifa kwa lengo la  kuwajengea uwezo wanamichezo wote.

Mbibo aliongeza kuwa wizara ina mpango wa kuwa na eneo maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi litakalojumuisha michezo yote pamoja na kuwepo na vifaa vyote vya michezo ili wanamichezo wa klabu ya madini waweze kupata uzoefu kabla ya kuingia katika mashindano.

Sambamba na hayo Mbibo amefafanua kuwa katika michezo motisha ni vyenzo muhimu ya ushindi hivyo Wizara itaendelea kutoa motisha kwa wanamichezo wote kwa jinsi itakavyowezekana nia kubwa ni kutoa hamasa kwa  wanamichezo.

Awali akitoa taarifa ya ushiriki Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Madini, John Issangu amesema kuwa klabu ya madini ilishiriki kwa ushindani mkubwa na kuweza kupata medali nne  ikiwamo ya Dhahabu moja, medali za fedha mbili na Shaba moja.


Akielezea juu ya ushindi huo Issangu amesema Medali hizo zilipatikana katika mchezo wa riadha kuanzia Mbio za mita 100 kwa washiriki kuanzia umri wa miaka 55-60 , medali ya fedha ilipatikana katika Mbio za mita 200 , medali ya tatu ambayo ya fedha ilipatikana  katika  mita 800 na medali katika mita 400.

Mashindano ya SHIMIWI ujumuhisha michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa Pete, kurusha tufe , mbio za baiskeli na michezo ya ndani kama vile Bao ,Draft na Karata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

Michezo

Unakosaje pesa ukiwa na Meridianbet leo

Spread the love Alhamisi ndio hii sasa mteja wa meridianbet ambapo leo...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

error: Content is protected !!