Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mikesha makanisani, mahubiri barabarani kutozwa kodi 334,600
Habari MchanganyikoTangulizi

Mikesha makanisani, mahubiri barabarani kutozwa kodi 334,600

Spread the love

BAADHI ya wahubiri na makasisi wamesema hatua ya serikali ya Kaunti ya Kisii nchini Kenya kuanza kutoza ushuru makanisa na wahubiri itarudisha nyuma injili. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Makanisa yanayofanya maombi ya mkesha wa usiku yatatakiwa kulipa KSh5,000 (Tsh 84,000) kila wiki baada ya Gavana Simba Arati atasaini Muswada wa Fedha wa Kaunti ya Kisii wa 2023, ambao tayari umepitishwa na Bunge la Kaunti hiyo.

Muswada huo unapendekeza kwamba makanisa yanayotaka kuendesha mkesha, yatalazimika kulipa ada hiyo.

Naye mhubiri yeyote atakayeingia mitaani kueneza Injili atalazimika kutenga KSh2,000 (Tsh 33,500)  kwa wiki ili aruhusiwe kuhubiri.

Ada ni kubwa zaidi kwa wahubiri ambao watatumia magari ya kubebea mizigo yenye vipaza sauti kwa sababu watahitajika kulipa hadi KSh20,000 (Tsh334,600) kwa wiki.

Baada ya muswada huo kupitishwa, baadhi ya makasisi wamejitokeza kulaani hatua ya uongozi wa kaunti kutaka kuwatoza.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wachungaji na Makasisi wa Kisii, Lawrence Nyanuga ametaja uamuzi huo kuwa wa kusikitisha na kumtaka Gavana Simba Arati kutouidhinisha hadi masuala yanayowagusa yatazamwe upya na kufanyiwa mabadiliko.

Kasisi Nyanuga alisema hatua hiyo ni usaliti wa hali ya juu zaidi ambao kanisa eneo la Kisii limepata kutoka kwa viongozi waliochaguliwa, waliokuwa wakiwatembelea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 kusaka maombi na uungwaji mkono kutoka kwa waumini wao.

“Sasa wamtugeuka na wanataka kututoza ushuru. Walipokuwa wakitafuta nyadhifa za uongozi, walikuwa wakituomba tuwaombee na kuwataka waumini kuwaunga mkono,” alisema mchungaji Nyanuga.

Badala ya kutoza makanisa kodi aliomba makanisa yaungwe mkono na serikali ili yawezeshwe kufikia nyoyo za watu wengi kwa njia ya uinjilisti.

“Katika hali nyingi, mkesha hazivutii watu wengi. Serikali ya kaunti inafikiri kwamba tunapata pesa kwa kufanya mikesha ya usiku lakini sivyo. Makanisa si mashirika ya kutengeneza faida,” alisema kasisi Nyanuga.

Huku makasisi hao wakishikilia kuwa kutoza ushuru makanisa ni sawa na kumtoza Mungu ushuru, wakazi wengine wa Kisii wamefurahia wakisema makanisa kulipa ushuru ni njia itakayosaidia kudhibiti wahubiri na makanisa yanayocheza muziki kwa sauti ya juu haswa katika maeneo ya makazi.

“Naunga mkono kikamilifu hatua ya watu wanaoendesha mikesha kulipa kodi. Kwa mfano, huwa sipati hata lepe la usingizi siku za Ijumaa katika sehemu ninayoishi kwa sababu ya sauti zinazoshindana kutoka kwa makanisa mbalimbali yaliyo hapo.

“Ninaipongeza Serikali ya Kaunti ya Kisii kwa kuja na pendekezo hilo ambalo kwa maoni yangu lilipaswa kuletwa mapema. Hili likishaanza kutekelezwa, nina uhakika litazima makanisa na maeneo mengine ya ibada kupiga muziki kwa sauti ya juu na hili litanipa fursa nzuri ya kupata usingizi mnono,” alisema Enock Ogoti, mkazi wa kiunga cha Daraja Mbili nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!