Monday , 20 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bilioni 16.2 kulipa fidia watakaopisha ujenzi barabara nchini
Habari za Siasa

Bilioni 16.2 kulipa fidia watakaopisha ujenzi barabara nchini

Spread the love

 

JUMLA ya Sh 16.2 bilioni zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi ambao watapisha ujenzi wa barabara mbalimbali nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Simiyu …(endelea).

Hayo yameelezwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu ya ukaguzi wa miradi ya barabara na kuzungumza na wananchi pamoja na wakandarasi.

Bashungwa alikagua utelelezaji wa ujenzi wa barabara ya mchepuo (Maswa Bypass) yenye urefu wa kilometa 11.3 kwa kiwango cha lami ambao ujenzi umefikia asilimia 99.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa lengo la Serikali la kuijenga barabara ya mchepuo ya Maswa (Maswa Bypass) ni kupunguza msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji wa Maswa.

Amesema Serikali tayari imetenga fedha kwa ajili ya kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa bararara ya Bariadi-Salama-Mhayo-Magu (km 76), Bariadi-Itilima-Mwandoya-Moroco (km 104), Nyashimo-Ngasamo-Ndutwa (km 48) ili kupata gharama za ujenzi wake kwa kiwango cha lami.

Akitoa taarifa ya mradi, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi John Mkumbo ameeleza kuwa mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa kati ya TANROADS na Mkandarasi kampuni ya CHICO tarehe 1 Juni, 2021 kwa gharam ya Sh 13.4 bilioni.

Ameongeza kuwa mkandarasi anaendelea kumalizia kazi ndogo ndogo za kuweka alama za barabarani, kuchora mistari ya usalama barabarani pamoja na kujenga miundombinu saidizi ya barabara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!