Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa WHO yaonya mlipuko homa ya Dengue
Kimataifa

WHO yaonya mlipuko homa ya Dengue

Spread the love

 

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limewataka wanachama wake kuchukua tahadhari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Dengue, unaodaiwa kusababishwa na ongezeko la joto duniani linalochochea ongezeko la mbu wanaosambaza virusi vyake. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tahadhari hiyo imetolewa na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka WHO, Jeremy Farrar, aliyetoa wito kwa mataifa kuanzisha mijadala ya kuweka mikakati ya kukabiliana na janga hilo.

Farrar amesema nchi zitakazoathirika na janga hilo katika muongo huu ni za kutoka Amerika ya Kusini, Ulaya Kaskazini na nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara, hususan katika miji yenye watu wengi.

“Tunahitaji kuzungumza zaidi kuhusu Dengue, tunahitaji kuandaa nchi juu ya namna zitakavyokabiliana na mlipuko unaokuja katika siku zijazo kwenye miji mingi mikubwa,” amesema Farrar.

Ugonjwa huo ulioathiri zaidi nchi za Asia na Amerika ya Kusini, unasababisha vifo takribani 20,000 kila mwaka, huku visa milioni 4.2 vikiripotiwa na mataifa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!