Saturday , 18 May 2024
Home Kitengo Michezo Taswa wampongeza Mobhare Matinyi
Michezo

Taswa wampongeza Mobhare Matinyi

Mobhare Matinyi
Spread the love

 

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kinampongeza Mobhare Matinyi kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uteuzi wa Matinyi aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa TASWA, umefanywa jana Oktoba mosi, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kabla ya uteuzi huo ulioanza mara moja, Matinyi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Matinyi ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa Habari na Mwanadiplomasia mbobevu aliyewahi kufundisha Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dk. Salim Ahmed Salim, Kurasini jijini Dar es Salaam aliwahi kuwa Mwenyekiti wa TASWA kwa mafanikio makubwa.

TASWA tunamtakia kila la kheri katika nafasi hiyo aliyoaminiwa na Mheswhimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia anastahili pongezi kwa uteuzi huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!