Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati Kuu CCM yamteua Bahati kuwa mgombea ubunge Mbarali
Habari za Siasa

Kamati Kuu CCM yamteua Bahati kuwa mgombea ubunge Mbarali

Spread the love

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan, imemteua wa Bahati Keneth Ndingo kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Uchaguzi huo mdogo wa ubunge umepangwa kufanyika tarehe 19 Septemba 2023, kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Francis Leonard Mtega aliyefariki dunia tarehe 1 Julai 2023.

Kamati hiyo imekutana leo Alhamis katika kikao chake maalum, kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma na kumteua Bahati ambaye sasa ni Mbunge wa Viti Maalumu CCM.

Aidha, Kamati Kuu ya CCM, imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Samia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Dk. Hussen Ali Mwinyi, kwa namna zinavyoendelea kuwatumikia wananchi kwa vitendo kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020- 2025.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!