WAKILI Philip Mwakilima ambaye anasimamia kesi inayomkabili ya Wakili Boniphace Mwabukusi na wenzie leo Alhamisi amesema mteja wake anaumwa hivyo Jeshi la Polisi limfikishe haraka mahakama pamoja na watuhumiwa wenzie ili wapate haki zao kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Wakili Mwakilima amesema mteja wake Mwabukusi ni mgonjwa, analala sakafuni huku akiwa na mishono mingi.
Bila kuutaja ugonjwa unaomsumbua Mwabukusi, Mwakilima ametoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata hilo huku akitoa wito kwa jeshi la polisi kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao.
Wakili Mwabukusi aliyekuwa anasimamia kesi ya kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba wa uwekezaji bandarini, Balozi Dk. Willibroad Slaa na Kada wa Chadema, Mpaluka Said Nyagali maarufu Mdude Nyagali walikamatwa kwa nyakati tofauti wiki iliyopita kwa tuhuma za uchochezi na uhaini.
Hayo yalijiri baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Camillius Wambura kuutangazia umma kuwa kuna watu wamepanga maandamano yenye uchochezi na malengo ya kupindua serikali.
Leave a comment