Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili aendelea kuhakiki vyama vya siasa
Habari za Siasa

Msajili aendelea kuhakiki vyama vya siasa

Spread the love

 

OFISI ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini, inaendelea na zoezi la uhakiki wa masharti ya usajili wa vyama hivyo, ambapo hadi sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha ACT-Wazalendo, vimefikiwa na zoezi hilo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Chadema kimefanyiwa uhakiki leo Alhamisi, tarehe 3 Agosti 2023,wakati ACT-Wazalendo, kikihakikiwa jana Jumatano.

MwanaHALISI Online, imemtafuta Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, ili kupata taarifa zaidi kuhusu zoezi hilo, ambaye amesema atatoa taarifa za awali kuhusu matokeo ya uhakiki huo kesho Ijumaa.

“Zoezi linaendelea na tayari Chadema na ACT-Wazalendo vimeshahakikiwa, kuhusu matokeo ya uhakiki nakushauri ungepiga kesho jioni maana tutakuwa tumeshamaliza wiki. Kwa sasa tunafanya uhakiki wa vyama vingine hivyo kesho itakuwa rahisi kufanya tathimini ya zoezi kisha kutoa taarifa ya awali,” amesema Nyahoza.

Mtandao ulimtafuta Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, kwa ajili ya kupata maoni yake kuhusu zoezi hilo, ambaye alijibu “wanaopaswa kusema ni ofisi ya msajili, nashauri ongeeni na msajili, sisi tukizungumza sasa haitakuwa vyema kuongea kabla wao hawajatoa matokeo ya uhakiki.”

Kwa mujibu wa ratiba ya zoezi hilo iliyotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, zoezi hilo linatarajiwa kufungwa tarehe 15 Agosti mwaka huu, ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitahakikiwa jijini Dodoma.

Ratiba hiyo inaonyesha orodha ya vyama vya siasa 19, vitakavyohakikiwa katika nyakati tofauti kuanzia tarehe 2 hadi 15 Agosti mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!