Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Uhaba wa dola wapaisha bei ya petroli
Habari MchanganyikoTangulizi

Uhaba wa dola wapaisha bei ya petroli

Spread the love

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia leo Jumatano, tarehe 2 Agosti 2023 saa 6:01 usiku huku zikiwa zimepanda ikilinganishwa na bei za mwezi uliopita.  Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Dar es Salaam ni kama ifuatavyo kwa lita: Petroli 3,199, Dizeli 2,935 na mafuta ya Taa 2,668.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo Jumatano, mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yanatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani na mabadiliko ya sera za kikodi.

Pia kupanda kwa mafuta hayo kumesababishwa na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

error: Content is protected !!