Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aitaka Serikali kutoa elimu kwa wanasiasa kuhusu mkataba DP WORLD
Habari za SiasaTangulizi

Zitto aitaka Serikali kutoa elimu kwa wanasiasa kuhusu mkataba DP WORLD

Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali itoe elimu kwa vyama vya siasa, kuhusu mkataba wa uwekezaji bandari nchini, ili kuondoa sintofahamu iliyokuwepo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Zitto ametoa wito huo leo Jumanne, jijini Dar es Salaam, akizungumza katika mkutano wa dharura wa Baraza la Vyama vya Siasa, ulioitishwa kwa ajili ya kujadili hali ya siasa nchini.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, sintofahamu iliyokuwepo sasa ndani ya vyama vya siasa kuhusu uwekezaji huo, inatokana na Serikali kutovipa elimu ya kutosha wadau wa vyama vya siasa, kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kiserikali kati yake na Serikali ya Dubai, kuhusu uendeshaji bandari nchini.

“Yote haya na mtikisiko uliotokea unaonyesha rangi zetu sisi kuwa sio wamoja tunajificha ficha, suala la bandari limeibua ukali wa maneno. CCM wameitisha kikao chao cha Halmashauri Kuu wamewaeleza wameelewa sasa wanatembea barabarani wanatoa ufafanuzi, lakini tatizo lililopo hakuna usimamizi mzuri wa kisiasa, hamfanyi jukumu lenu la msingi mnaingiza watu kwenye tatizo,” amesema Zitto.

Kauli ya Zitto imetokana na mjadala wa sakata la bandari kuibuliwa ndani ya mkutano huo, ambapo baadhi ya watu walionesha kukasirishwa na baadhi ya vyama vya siasa vinavyotumia lugha zisizo za staha dhidi ya viongozi wa Serikali wakati wanawasilisha hoja zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!