Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Majeshi ya Urusi yadai kuua majenerali Ukraine
Kimataifa

Majeshi ya Urusi yadai kuua majenerali Ukraine

Spread the love

JESHI la Urusi lililopo katika operesheni maalum nchini Ukraine limedai kuwaua majenerali wawili katika shambulizi la mapema wiki hii. Anaripoti Joseph Nyoni kwa msaada wa mitandao…(endelea).

Gazeti la The Moscow Times limeeleza kuwa, pamoja na kuwaua majenerali hao, majeshi ya Urusi pia yamedai kuwaua maafisa 50 wa jeshi la Ukraine.

Hali hiyo imeelezwa kuwa inaendelea kuipa mtihani Ukraine, nchi ambayo imekuwa ikielemewa na mashambulizi makali kutoka kwa majeshi ya Urusi huku majenerali na maafisa wake wakubwa wa jeshi wakizidi kupoteza maisha.

Shirika la habari la RIA liliripoti kwamba  majenerali hao pamoja na maafisa 50  wa jeshi la Ukraine waliuawa katika mji wa Mashariki wa Kramatorsk nchini Ukraine tarehe 27 Juni mwaka huu.

Moscow pia imeeleza kuwa jaribio uasi lililofanywa na Wagner Yevgeny Prigozhin nchini Urusi halitaathiri operesheni za Urusi nchini Ukraine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!