Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini
Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the love

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston Lusinde amesema CCM haina mpango wakuliachia jimbo la Moshi mjini pamoja halmashauri ya Manispaa hiyo kwa vyama vya upinzani. Anaripoti Safina Sarwatt,Moshi…(endelea).

 

Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo(CCM)

Lusinde ambaye ni Mbunge wa Mtera mkoani Dodoma ameyasema hayo jana tarehe 31 Mei 2023 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, ulioandaliwa na Mbunge wa Moshi mjini, Priscus Tarimo na kufanyika katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi mjini Moshi.

Kauli hiyo ya Lusinde imekuja baada ya jimbo hilo kuwa mikononi mwa NCCR Mageuzi ma Chadema kwa kipindi cha miaka 25 kuanzia mwaka 1995 hadi 2020.

Historia inaonyesha uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, Jimbo la Moshi lilichukuliwa na Joseph Mtui wa NCCR-Mageuzi na baadae akaja Philemon Ndesamburo (2000-2015) na kurithiwa na Jaffar Michael wa Chadema pia.

Ndesamburo ambaye alikuwa mmoja wa waasisi wa Chadema na mfadhili wa chama, alikuwa na kadi ya uanachama namba 10 na ndiye alikuwa mwiba na alikuwa na uwezo wa kuvuruga mipango ya CCM.

Aidha, akihutubia wananchi katika mkutano huo, Lusinde amesema CCM bado ni chama bora duniani kuliko vyama vyote vya siasa kwani inafanya yale ambayo ni matakwa ya wananchi hivyo huwezi kuifananisha hivo vya vyama vingine vinavyoibuka ibuka huko na haivina sera..

Amesema CCM imeendelea kutekeleza yale yote yaliahidiwa katika ilani ya uchaguzi ambayo ndiyo mahitaji muhimu ya wananchi ikiwemo maji, afya, elimu, umeme kwa asilimia kubwa nchi nzima.

Katika hatua nyingine Lusinde ameeleza kukerwa na vitendo vya kukamata pikipiki na  kuwekwa katima kituo cha polisi kwa muda mrefu bila sababu za msingi kama zile zilizohusika kwenye makosa ya jinai.

“Wako maaskari wazuri lakini tuwajengee uwezo na wale ambao wanawavunjia heshima askari tuwachukulie hatua,”amesema.

Lusinde amewataka viongozi kukema vitendo vya ukatili pamoja na nidhamu kwa viongozi katika ngazi zote.

Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo(CCM) amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan miradi mingi imetekelezwa.

Amesema miradi iliyotekelezwa ni pamoja na  ujenzi mradi wa jengo la huduma ya mama na mtoto katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi lililogharimu zaidi ya Sh 6 bilioni.

Amesema  katika bajeti ijayo imepitishwa Sh tatu bilioni kwa ajili ya kujenga wodi za kisasa za ghorofa  hospitali hiyo, ili ifanane na hospitali za mikoa zenye hadhi.

“Sekta ya elimu  tumejenga shule mpya ya sekondari katika eneo la Msandaka kwa gharama ya Sh 570 milioni, na halmashauri imetenga Sh 150 milioni kwa ajili ya mabweni ya shule hiyo ambapo pia tunakusudia kuyaweka kwa ajili ya kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule ya Sekondari Mawenzi,” amesema.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi, Zuberi Kidumo ameema katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia, Manispaa hiyo wamepokea zaidi ya Sh21 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!