Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu
Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love

 

IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha sukari cha Bagamoyo, siyo sehemu ya shamba linalomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ambalo wanataka waliolivamia, waondoke mara moja. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI leo Alhamisi, tarehe 1 Juni 2023, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Charles Hilary anasema, eneo ambalo Serikali Visiwani inadai kuwa ni mali yake, halina uhusiano wowote na mahali ambako kumejengwa kiwanda cha sukari cha Bagamoyo.

Kiwanda cha sukari cha Bagamoyo na mradi wa shamba la miwa, unaofahamika kwa jina la “Bagamoyo Sugar Project,” unamilikiwa na mmoja wafanyabiashara mashuhuri nchini, Said Salim Bakharesa.

Mkurugenzi huyo wa mawasiliano Ikulu, alikuwa akijibu maswali ya mwandishi wa gazeti hili, aliyetaka kufahamu, ikiwa ardhi wanayodai kuwa ni mali yao, ndiko kumejengwa kiwanda cha sukari cha Bakharesa, na ikiwa ni hivyo, hawaoni kuwa wanaibua kero nyingine ya Muungano.

Alisema, “hapana. Ni sehemu tofauti kabisa na kule kwa Mzee Bakharesa. Tunapokuzungumzia sisi, ni lile eneo ambalo limevamiwa na matapeli wanaowauzia wananchi na kuwaambia wajenge kwa haraka.”

Aliongeza, “hakuna mgogoro utakaotokea. Hakuna mgogoro wowote uliopo au utakaotokea, kati ya serikali hizi mbili. Utoaji wa eneo hilo kwa muwekezaji umeridhiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.”

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Charles Hilary

Alipoulizwa kwa nini wametoa kauli hiyo sasa wakati tayari eneo kubwa limejengwa makazi na wananchi, mkurugenzi huyo alisema, “tumeamua kuwapa taarifa wale wanaomilikishwa maeneo hayo, kupitia matapeli ambao wanayatangaza kwamba yanauzwa.”

Alipoombwa majina ya waliovamia maeneo yao, Charles alisema, “hatuna orodha kamili. Lakini taarifa za udanganyifu kutoka kwa hao matapeli wanavyoyanadisha maeneo yetu, tunayo huku wakiwasisitiza wanunuzi wafanye ujenzi haraka.”

MwanaHALISI lililazimika kumtafuta msemaji huyo wa Ikulu, kufuatia kuibuka kwa taarifa kuwa shamba ambalo serikali ya Zanzibar inasema inalimiki huko Makulunge, wilayani Bagamoyo, lilishatolewa na Serikali ya Muungano kwa muwekezaji na tayari kumejengwa kiwanda cha sukari.

Haya yalijiri siku moja baada ya serikali Visiwani, kuutangazia kuwa shamba hilo lililokuwa likifahamika kama ranchi ya Zanzibar-Bagamoyo (Razaba), lililopo katika kijiji cha Winde kata ya Makulunge, ni mali halali ya serikali hiyo.

Katika taarifa yake, serikali ilisema, shamba hilo lenye ukubwa wa takribani hekta elfu sita, ni mali ya SMZ, tangu mwaka 1977 na kwamba haimtambui mtu yoyote aliyemilikishwa; na au kujimilikisha eneo hilo.

Aliongeza: “Hivyo ni marufuku kwa mtu, taasisi au kikundi chochote, kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi cha watu, kitakachokwenda kinyume na tangazo hilo.”

Said Salim Bakharesa

Aidha, taarifa ya serikali ilisema, SMZ haitakuwa na wajibu wa kulipa fidia kwa mtu yoyote aliyepatiwa eneo katika shamba lake.

Mgogoro kati wananchi wa kijiji cha Winde na Ranchi ya Razaba, umedumu kwa zaidi ya miaka 40 sasa, kufuatia baadhi yao kudai kuwa eneo lao lilichukuliwa na Serikali ya Zanzibar, bila ridhaa yao na bila kuwalipa fidia.

 Lakini Razaba wanadai kuwa kabla ya kulichukua eneo hilo, ambalo lilikuwa likitumika kwa ajili ya kufungia ng’ombe kabla ya kusafirishwa Zanzibar, walilipa mamilioni ya fedha kama fidia kwa wananchi hao.

Ranchi ya Razaba ilianzishwa Oktoba mwaka 1977 kwa makubaliano ya pande mbili kati ya Serikali ya Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambapo jumla ya  hekari 77,663 zilikabidhiwa kwa serikali ya Visiwani, kupitia iliyokuwa wizara ya kilimo na maliasili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!