Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Balozi Shelukindo ateta na mabalozi China, Italia, Denmark…
Habari za Siasa

Balozi Shelukindo ateta na mabalozi China, Italia, Denmark…

Spread the love

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo amekutana na kuzungumza na mabalozi wa China, Kenya, Denmark, Italia na Sudan kwa nyakati tofauti na kujadiliana nao masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mabalozi waliokutana na Balozi Shelukindo ni Balozi wa China, Chen Mingjian; Balozi wa Kenya, Isaac Njenga; Balozi wa Norway, Mette Norgaard Dissing-Spandet; Balozi wa Italia, Marco Lombard na Kaimu Balozi wa Sudan, Asim Mustafa Ali.

Dk. Shelukindo amekutana na mabalozi hao katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili na kuahidi kuongeza ushirikiano katika sekta za elimu, michezo, biashara na uwekezaji.

“Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na China, Kenya, Denmark, Italia na Sudan ambapo uhusiano huo umesaidia kuwa na misingi imara ya ushirikiano kwa maslahi mapana ya Taifa letu na nchi zao,” alisema Dk. Shelukindo.

“Vilevile nimepata fursa ya kukutana na Balozi wa Sudan na amenijulisha juu ya uwezekano wa mapigano yanayoendelea nchini humo kufikia mwisho kwa njia ya makubaliano. Na amenihakikishia kuwa wanafunzi waliokuwa wanasoma nchini Sudan watapokelewa na kuendelea na masomo yao baada ya mapigano kumalizika.

Amesema tarehe 11 Mei, 2023 pande zinazopigana nchini humo zilisaini mkataba wa makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano,” alisema Dk. Shelukindo.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Sudan nchini, Mustafa Ali amemhakikishia Katibu Mkuu kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumalizika kwa mapigano yanayoendelea nchini humo kwa njia ya makubaliano ya amani.

“Naomba nikuhakikishie kuwa Serikali ya Sudan itawapokea wanafunzi waliokuwa wanasoma nchini kwetu na kupata fursa ya kuendelea na masomo yao baada ya mapigano kumalizika,” alisema Mustafa Ali

Naye Balozi wa China nchini, ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono China na kuahidi kuendeleza harakati za kusaidia nchi zinazoendelea na kuongeza kuwa China itaendelea kuisadia Tanzania katika kufanikisha miradi mbalimbali ya kimkakati.

Kwa nyakati tofauti mabalozi hao  wameishukuru Tanzania kwa ushirikiano mzuri ambao wamekuwa wakiupata wakati wa utekelezaji wa majukumu yao na kuahidi kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya pande zote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!