Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania yalaani mapigano Sudan, kuwarejesha nyumbani Watanzania 210
Habari za Siasa

Tanzania yalaani mapigano Sudan, kuwarejesha nyumbani Watanzania 210

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imezitaka pande mbili zinazosigana nchini Sudan na kusababisha mapigano yaliyogharimu maisha ya watu zaidi ya 180 na majeruhi 1,000, ziketi mezani kwa ajili ya kutafuta muafaka kwa njia ya amani na usalama. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 19 Aprili 2023, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax, akitoa msimamo wa Tanzania kuhusu mapigano hayo yaliyoibuka tarehe 15 Aprili mwaka huu, kati ya vikosi vya Serikali na vikosi vya misaada.

Dk. Tax amesema, Tanzania inaunga mkono tamko lililotolewa na Baraza la Amani la Usalama la Umoja wa Afrika (AU), lilitolewa tarehe 16 Aprili 2023, kulaani mapigano hayo ambayo yalisitishwa kwa saa 24 kuanzia jana jioni.

“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaunga mkono tamko lililotolewa na Baraza la Amani la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani mapigano yanayoendelea Tanzania, inazitaka pande zote mbili zinazohasimiana kutatua mgogoro huo kwa njia ya amani na usalama, huku ikihakikisha haki na usalama wa raia,” amesema Dk. Tax.

Waziri huyo wa mambo ya nje, amesema hakuna mtanzania aliyepoteza maisha au kujeruhiwa, huku akisema Serikali inafuatilia ili kuandaa mpango wa kuwaondoa raia wa Tanzania nchini humo kama hali haitakuwa shwari.

“Tunao Watanzania takribani 210, hadi sasa hakuna Mtanzania aliyeripotiwa kujeruhiwa na mapigano hayo. Serikali inachukua hatua kuhakikisha watanzania wanakuwa salama na tunaendelea na juhudi hii. Hadi sasa mapigano yamesitishwa kwa saa 24 kuanzia jana jioni kutoa fursa za mahitaji ya kibinadamu,” amesema Dk. Tax na kuongeza:

“Kufuatia juhudi zinazoendelea uko uwezekano na muelekezo uliopo ni kusitisha mapigano kutatua mgogoro kwa amani, Serikali inafuatilia kuandaa mpango wa kuwachukua raia wa Tanzania kadri itakavyohitajika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!