Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wagombea Uchaguzi TLS watangazwa, kampeni kuanza Machi 27
Habari Mchanganyiko

Wagombea Uchaguzi TLS watangazwa, kampeni kuanza Machi 27

Wakili Msomi Harold Sungusia
Spread the love

 

KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), imetangaza majina ya walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Mei 2023. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Majina hayo yametangazwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TLS, Charles Rwechungura, baada ya kamati hiyo kuketi kuanzia tarehe 18 hadi 20 Machi mwaka huu, kwa ajili ya kufanya mchujo wa majina ya waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali.

Kwa mujibu wa majina hayo yaliyotangazwa hivi karibuni, walioteuliwa kugombea nafasi ya Urais wa TLS, ni Mawakili Wasomi, Harold Sungusia na Reginald Shirima.

Awali waliotia nia walikuwa watatu ambapo jina la Sweetbert Nkuba, lilishindwa kupenya katika mchujo kutokana na kutokidhi vigezo ikiwemo kuwa mtumishi wa umma na kutofanya shughuli za uwakili katika kipindi cha miaka 10.

Wagombea hao wawili waliopenya, watachuana kugombea nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Prof. Edward Hoseah, anayemaliza muda wake.

Kwa upande wa nafasi ya makamu wa rais wa TLS, waliopitishwa kugombea nia, Revocatus Kuuli, Emmanuel Augustino, Aisha Sinda na Fredrick Mtei, huku katika nafasi ya mweka hazina akipitishwa Christopher Mageka, kugombea.

Katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Vijana, aliyepitishwa kugombea ni Wakili Edward Heche, baada ya aliyekuwa mpinzani wake, Emanuel Nyanza, kuomba kujitoa.

Mawakili Peter Mabiki na Samwel Banzi, wamepitishwa kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa chama hicho, huku Susan Reuben akipitishwa kugombea nafasi ya ukatibu.

Taarifa iliyotolewa na Rwechungura, inasema kampeni za uchaguzi huo zitafanyika kuanzia tarehe 27 Machi hadi 11 Mei 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!