Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wanajeshi Namibia watembelea TRC, waimwagia sifa SGR
Habari Mchanganyiko

Wanajeshi Namibia watembelea TRC, waimwagia sifa SGR

Spread the love


SHIRIKA la Reli Tanzania  (TRC) limepokea ugeni wa wanafunzi wanajeshi wanaoshiriki kozi ya ukamanda na unadhimu kutoka nchini Namibia ambao wametembelea ujenzi wa mradi reli ya kisasa – SGR kipande cha kwanza Dar es Salaam – Morogoro kwenye jengo la stesheni ya jDar Es Salaam Machi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wanafunzi hao wametembelea ujenzi wa mradi wa SGR ili kujionea maendeleo na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama katika miundombinu ya mradi huo mkubwa wa kimkakati.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema ujenzi wa SGR ni maono ya Tanzania katika kuunganisha nchi hiyo na Afrika Mashariki na mbali zaidi kuziunganisha nchi zote za Afrika kupitia reli ili kuleta maendeleo na kuwaunganisha watu.

“Ujenzi wa reli hii ya kisasa ni maono ya viongozi wetu wa Afrika waliotangulia na wa sasa, katika kuleta maendeleo ya haraka na kwa pamoja lazima sekta ya uchukuzi iendelee, ili kuziunganisha nchi na watu wake kwa pamoja.

“Lazima tuwe na miundombinu thabiti itakayoweza kuwatoa watu sehemu moja na kuwaleta sehemu nyingine kwa haraka na kwa wingi, miundombinu itakayowezesha sekta nyingine kukua kwa haraka kama vile kilimo na viwanda, ndipo wazo la ujenzi wa SGR lilipotokea” alisema Kadogosa.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu  huyu ameongeza kuwa sekta ya uchukuzi inachangia pato la Taifa kwa takribani asilimia 14 ukilinganisha na sekta nyingine, hivyo ujenzi wa SGR kwa namna moja au nyingine utaenda kuongeza maradufu pato la Taifa ikizingatiwa kuwa hivi karibuni mwezi Mei, 2023 shughuli za usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro zitaanza na baadaye mwezi Septemba, 2023 treni kutoka Morogoro hadi Makutupora zitaanza.

“Sekta ya uchukuzi ni nyeti sana, sekta hii inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 14, sekta hii ni chachu katika kukuza sekta nyingine kama kilimo, huwezi kulima mazao mengi kama huna usafiri wa kuyapeleka sokoni, viwanda haviwezi kukua bila uchukuzi , wafanyakazi hawawezi Kwenda makazini bila usafiri, kwahiyo kwa namna hii SGR itakapoonza hivi karibuni tunatarajia Mei mwaka huu, tutaenda kuona mabadiliko katika kiuchumi” alisema Kadogosa.

Naye Mkufunzi Mkuu wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu ambaye pia ni Mkuu wa Msafara kutoka nchini Nambia Kanali Linanga amelipongeza Shirika la Reli Tanzania kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa SGR na kupitia historia ya reli ya Tanzania wametambua maono ya viongozi ambayo yameweza kuleta mabadiliko na maendeleo katika sekta ya reli hadi kufikia ujenzi wa mradi mkubwa wa kimkakati wa SGR.

“Tumeona, tumejifunza mengi sana kutoka katika historia ya reli mpaka sasa kwa kweli haya ni mapinduzi, reli hii imekidhi haja ya kila mmoja, itawafaa watu wote wenye kipato kikubwa na wa hali ya chini, wote tutasafiri kwa kutumia treni hii, tutaenda kusimulia tukifika Namibia kwamba tumeona mapinduzi alisema Kanali Linanga.

Pindi shughuli za undeshaji wa treni za SGR utakapoanza, Shirika la Reli litatoa fursa kwa watu binasfi, mashirika na makampuni kuwekeza ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji na kuongeza pato la nchi na mtu mmoja mmoja

1 Comment

  • KWA AJILI YA MASHINDANO YA MTU WA KWANZA KUWAHI PATIKANA DUNIANI – UKIONA VIPI TUMA KWENYE ANUANI HII

    H.E Ambassador
    Dr. Emmanuel John Nchimbi
    The Embassy of the United Republic of Tanzania
    10 ANAS Ibn Malek Street,
    Mohandessin,
    Cairo, Egypt
    Postal Code: 12411

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!