Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Marekani yataja sababu Kamala Harris kutua nchini
Habari za SiasaKimataifa

Marekani yataja sababu Kamala Harris kutua nchini

Spread the love

SERIKALI ya Marekani imesema ziara ya Makamu wa Rais wa Taifa hilo, Kamala Harris kwa nchi za Afrika ikiwamo Tanzania, ni kujadili vipaumbele vya dunia kwa sasa ambavyo ni demokrasia, uchumi shirikishi, usalama wa chakula na madhara ya Urusi kuivamia Ukraine. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Harris na msafara wake unatarajia kuanza ziara Barani Afrika kuanzia tarehe 25 Machi hadi tarehe 2 Aprili mwaka huu kwa kutembelea nchi tatu ambazo ni Tanzania, Ghana na Zambia.

Katika ziara hiyo, Makamu huyo wa Rais atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema pamoja na Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani

Katika taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Machi 2023 na Ikulu ya Marekani, imesema, ziara hiyo inalenga kuboresha ushirikiano kati ya Marekani na nchi za Afrika kwa kuzingatia masuala ya usalama na uchumi endelevu.

Ziara hiyo ambayo pia itahusisha mazungumzo na wadau wa sekta binafsi, inalenga kujadili namna ya kuenenda na mabadiliko ya ukuaji wa uchumi kidijitali, mabadiliko ya tabianchi, uwekezaji, mazingira ya kibiashara na ujasiriamali sambamba na kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Harris ambaye ni Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke katika taifa la Marekani, ujio wake unahisiwa kuwa huenda ukawa ni maandalizi ya ziara ya Rais wa Marekani, Joe Biden aliyoahidi kuifanya Afrika mwaka huu.

Itakumbukwa kuwa Aprili 2022, Rais Samia alikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa taifa hilo, Kamala Harris jijini Washington.

Kamala Harris ambaye ni makamu wa 49 wa Marekani na yeye sasa anafanya ziara yake ya kwanza nchini Tanzania.

Marais wa Marekani ambao hadi sasa wameitembelea nchi ya Tanzania ni pamoja na Bill Clinton, George Bush, pamoja na Barack Obama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!