Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yakadiria bajeti ya Sh 44.3Tril. mwaka 2023/24
Habari Mchanganyiko

Serikali yakadiria bajeti ya Sh 44.3Tril. mwaka 2023/24

Spread the love

 

SERIKALI imewasilisha kwa Wabunge Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, ambapo imepanga kukusanya na kutumia jumla ya Sh. 44.3 trilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu Dodoma … (endelea).

Bajeti hiyo inajumuisha Sh. 29.2 trilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh 15.1 trilioni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Akiwasilisha mapendekezo hayo leo Jumatatu tarehe 13 Machi, 2023 jijini Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema kiasi hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 7 ikilinganishwa na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge ya mwaka wa Fedha 2022/23 ya Sh. 41.5 trilioni.

Amesema jumla ya mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Sh. 31 trilioni , sawa na asilimia 70.7 ya bajeti yote ambapo kati ya mapato hayo, mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 13.0 hadi Sh. 26.7 trilioni kutoka makadirio ya Sh.23.7 trilioni mwaka 2022/23.

“Misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo inatarajiwa kufikia Sh. 5.4 trilioni, sawa na asilimia 12.3 ya bajeti yote,” amesema Dk. Nchemba.

Dk. Nchemba amesema Serikali inatarajia kukopa Sh. 5.4 trilioni kutoka soko la ndani ambapo Sh. 3.5 trilioni ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na Sh. 1.9 trilioni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Ameongeza kuwa Serikali inatarajia kukopa Sh. 2.1 trilioni kutoka soko la nje kwa masharti ya kibiashara ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu.

Kuhusu mgawanyo wa matumizi, Dk. Nchemba alisema kuwa kati ya fedha hizo, Sh. 29.2 trilioni zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikijumuisha Sh. 12.8 trilioni kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama nyingine za Mfuko Mkuu na Sh. 10.9 trilioni kwa ajili ya mishahara ikiwemo upandishaji wa madaraja kwa watumishi na ajira mpya, na Sh. 6.4 trilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC).

“Matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 15.1 ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 11.9 ni fedha za ndani, sawa na asilimia 78.3 ya bajeti ya maendeleo na shilingi trilioni 3.2 ni fedha za nje”, ameongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!