MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha, ameitaka Serikali kurekebisha vifungu vinavyozuia vijana wenye umri chini ya miaka 20 kugombea nafasi za uongozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kamugisha ametoa wito huo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), jana tarehe 12 Machi 2023.
Alisema kuwa, Sheria ya Uchaguzi imemnyima kijana mwenye umri kuanzia miaka 18 hadi 20 kupigiwa kura, wakati mwenye umri kuanzia miaka 18, anaruhusiwa kupiga kura.
“Sheria ya Uchaguzi inamtaka kijana mwenye umri wa miaka 18 kupiga kura lakini inamnyima haki ya kupigiwa kura kwa maana kugombea ubunge na udiwani hadi ufikie umri wa miaka 21. Vijana wengi wenye uwezo na sifa za kuwa kiongozi kuwa nyuma ya wagombea kuwachorea ramani na mikakati ya ushindi,” alisema Kamugisha.
Mwenyekiti huyo wa vijana ACT-Wazalendo Dar es Salaam, amewataka vijana kupaza sauti zao ili mfumo unaotenga katika uongozi uondolewe.
Amewaasa wanafunzi hao wanaotaka uongozi, kuwa wasikivu, welevu, wavumilivu, wafuatiliaji na wapanga mikakati.
Kamugisha amewataka vijana wanaotaka uongozi, kujitenga na matumizi ya nguvu, umaarufu na mafanikio ya haraka.
Leave a comment